Meli ishirini na tano zitakuwa zinapiga doria katika pwani ya mji huo.
Huku hayo yakijiri, Ujerumani inajiandaa kushuka dimbani katika fainali ya Kombe la Dunia katika uwanja wa Maracana Brazil, dhidi ya Argentina huku ikipigiwa upatu kumzidi nguvu mpinzani wake huyo wa Amerika ya Kusini.
Katika mechi tatu za mwisho ambazo timu hizo zimekutana, Wajerumani ndio
walioibuka washindi. Ujerumani ilishinda katika fainali ya 1990 mjini
Rome 2-1 na kuwa bwaga Argentina katika robo fainali za
Kombe la Dunia 2006 kupitia mikwaju ya penalti mjini Berlin, na tena ikawachabanga
magoli manne kwa sifuri katika robo fainali miaka minne iliyopita mjini
Cape Town, Afrika Kusini. Nayo Argentina iliipiku
iliyokuwa Ujerumani ya Magharibi magoli matatu kwa mawili katika fainali
ya 1986 mjini Mexico City.
Brazil inachuana na Uholanzi hii leo.AidhaLoius Van Gaal, kocha wa Uholanzi anasema mchuano huu huwa hauna maana. Mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu kwa kawaida huwa siyo maarufu, na kivumbi cha leo mjini Brasilia kitakuwa tu cha kuwaliwaza wenyeji Brazil ambao bado wana maruweruwe ya kichapo walichopewa na Ujerumani.
Said PiePie,Nairobi.
Huku hayo yakijiri, Ujerumani inajiandaa kushuka dimbani katika fainali ya Kombe la Dunia katika uwanja wa Maracana Brazil, dhidi ya Argentina huku ikipigiwa upatu kumzidi nguvu mpinzani wake huyo wa Amerika ya Kusini.
![]() |
Kikosi chaUjerumani katika kambi ya maandalizi |