Wednesday, 25 June 2014

SUAREZ AMNG'ATA GIORGIO


 
Luiz Suarez aendeleza ukandamizaji
                   Strika wa  Uruguay Luis Suarez anakabiliwa na marufuku  itakayomlazimu kukosa mechi nyengine za michuano ya kombe la dunia iwapo atapatikana na hatia ya kumng'ata mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini katika mechi ya hapo jana.

Shirikisho la soka duniani FIFA limeanzisha uchunguzi wa kumuadhibu mcheza huyo kufuatia ushindi wa moja kwa bila dhidi ya Italy.
Chiellini amedai kwamba Suarez alimng'ata bega lake licha ya Suarez kudai kuwa ni mchazaji huyo aliyemchezea vibaya.

Giorgio Chiellini aonyesha jeraha baada ya kung'atwa na Suarez
  

Suarez mwenye umri wa miaka 27 huenda akapigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi 24 ama miaka miwili.
Refa aliyesimamia mechi hiyo kutoka Mexico Marco Rodriguez hakuchukua hatua yoyote kufuatia kisa hicho,lakini FIFA bado inaweza kumuadhibu Suarez.
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Liverpool Jan Molby anatarajia kwamba Suarez atapigwa marufuku kwa mechi zote za kombe hilo zilizosalia.



Said PiePie,Nairobi.

LAMOUCHI AGURA IVORY COAST



Aliyekua kocha wa Ivory Coast Sabri Lamouchi


        Kocha wa Ivory Coast Sabri Lamouchi amejiuzulu baada ya timu yake kuzabwa 2-1 na Ugiriki hapo jana katika mechi ya kuisismua
Lamouchi aliliambia jarida la AFP katika mahojiano jana baada ya mechi hiyo kumalizika aidha raia huyo wa Ufaranza mwenye umri wa mika 42 amesema kuwa kandarasi yake ilimalizika jana.
Hata hivyo amedokeza kuwa kushindwa kwake kulichangiwa na mchezo duni ambao wachezaji wake walionyeshwa baada ya kupoteza fursa tumbi nzima waliopata.Lamouchi ilianza kuwaongoza Ivory Coast mnamo Mei 2012.

Said PiePie,Nairobi.




MECHI ZA KPL ZAHAIRISHWA


                             

        Mechi saba za ligi ya primia humu nchini  zilizokuwa zimeratibiwa kusakatwa wikendi hii zihairishwa.Kulingana na afisa mkuu ya Ligi ya primia nchini Jack Oguda amesema kuwa hali hii imechangiwa na kusafiri kwa kikosi cha Harambee Stars  kuelekea Brazil
Aidha Oguda ameongeza kuwa michuano ya ligi ya primia itarejelewa kuanzia Jumamosi tarehe 5 Julai na Jumapili 6 mwezi ujao.


Said PiePie,Nairobi.