Tuesday, 1 July 2014

"RAMADHAN HAIKUTUADHIRI" ALGERIA WAKIRI.


 
Mlindalango wa Algeria Rais M’Bolh
      Rais M’Bolhi golkipa wa Algeria amekanusha madai wachezahi wao walishindwa na Ujerumani kutokana na wao kuwa wadhaifu kwa kufunga saumu.M’Bolhi ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo ambayo Algeria walishindwa mabao 2-1 na Ujerumani katika muda wa ziada anasisitiza kuwa Saumu hakikuchangia kwao Kushindwa.Aidha M’Bolhi anasema kuwa wachezaji hao wamekwisha zoea kucheza hata wakiwa kwenye mfungo na hivyo haipaswi kutolewa kama sababu .Kabla ya mechi hiyo kulikuwa na ubishi baada ya kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic kukataa kuulizwa maswali kuhusiana na mfungo wa Ramadhan ambao ulikuwa umeanza jumamosi .Halilhodzic alikataa kufichua idadi ya wachezaji wake ambao wanafunga mfungo wa Ramadhan kabla ya mechi .Wakati uo huo kocha huyo alikataa kujibu swali ikiwa wachezaji wake watafunga Ramadhan au la wakati wakicheza.Kulingana na dini ya Kislamu ,Ramadhan ni nguzo muhimu ya dini na ifikapo wakati huo kila mtu mwenye umri wa baleghe hujinyima chakula kuanzia alfajiri hadi magharibi .Hiyo inaamisha kuwa wachezaji wa Algeria hawakuwa wamekula chochote hadi baada ya kipindi cha pili cha mechi hiyo ndipo waliporuhusiwa  kunywa na  kula .Ujerumani ilifuzu kwa robo fainali ya kombe la dunia ambapo watakutana na Ufaransa ijumaa ijayo.

Said PiePie,Nairobi.

No comments:

Post a Comment