Klabu za ligi kuu ya soka nchini England zimeafikiana kutumia teknolojia ya camera katika maamuzi ya mchezo wa soka
kuanzia msimu ujao.
Kampuni ya Uingereza ya Hawk-Eye imepewa mkataba wa kufunga vifaa maalumu kwenye viwanja vyote 20
vya timu za ligi kuu nchini England.
Hawk-Eye inajulikana kwa
teknolojia kama hiyo kwenye mchezo wa Tenesi na Kriketi,ambapo camera
maalumu huweza kutambua iwapo mpira umegusa mstari ama la na kumjulisha
mwamuzi na wasaidizi wake ndani ya sekunde chache.
Chama cha soka nchini England FA,kitafunga vifaa
hivyo kwenye uwanja wa Wembley tayari kwa kutumika kwenye mchezo wa
ngao ya jamii hapo mwezi wa nane mwaka huu.
Viwanja vya timu 17 zitakazosalia ligi kuu na
zile 3 zitakazopanda daraja vitawekewa teknolojia hiyo na shughuli
nzima itachukua wiki sita kukamilika.Msukumo wa kutumia teknolojia maalumu ya
kutambua goli ilipata nguvu baada England kukataliwa goli lao la
kusawazisha walipocheza na Ukraine,Mchezo ambao England walifungwa bao
moja kwa bila kwenye michuano ya kombe la mataifa barani Ulaya mwaka
2012, Ambapo mwezi mmoja baadaye bodi ya vyama vya soka vya kimataifa
(IFAB) katika kikao chake mjini Zurich kilipitisha teknolojia mbili ili
zitumike kwenye michezo ya soka.Rais wa FIFA
Sepp Blater amesema kukataliwa kwa goli la Frank
Lampard kwenye mechi ya robo fainali kati ya England na Ujerumani mwaka
2010 katika michuano ya kombe la dunia,kulichangia kwa kiasi kikubwa
maamuzi ya shirikisho hilo kupitisha sheria ya matumizi ya teknolojia ya
kutambua goli.
Chama cha soka cha England kimesema teknolojia hiyo itaaanza kutumika msimu ujao.Kwa sasa Goal Technology inatumika katika michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.
Said PiePie,Nairobi.