Tuesday, 8 July 2014

BRAZIL KUMENYANA NA UJERUMANI KWENYE NUSU FAINALI

    
Kikosi cha Brazil kikinoa makali
      M
linzi  wa Brazil Thiago Silva hatocheza katika mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani Jumanne.Licha ya  juhudi za shirika la soka la Brazil kukata rufaa kwa shirikisho la soka duniani FIFA kutaka kadi ya pili ya njano iliyompelekea kupigwa marufuku mechi hiyo muhimu kuambulia patupu.Fifa imepuzilia mbali ombi la BFA la kuitaka ibatilishe kadi ya njano ambayo imemlazimu kocha Luiz Felipe Scolari kutafuta mlinzi mbadala kuziba pengo la nahodha huyo.
Thiago alionyeshwa kadi yake ya pili timu hiyo ilipoilaza Colombia Ijumaa iliyopita.
wakati uo huo Brazil wamepata pigo kwani Mshambuli machachari Neymar ambaye alijeruhiwa      uti wa mgongo.Kocha wa Brazil Scolari anapanga kutumia Willian kuziba pengo la Neymar.Scolari amesema kuwa Brazil itajitahidi dhidi ya Ujerumani licha ya kumkosa Neymar ambaye alikuwa ameifungia mabao manne.Aidha  kocha wa Ujerumani Joachim Low amesema kuwa Samba boys ni wakakamavu na wana jituma katika safu zao mbalimbali.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Ujerumani


 Low amemtaka refarii wa Mexico Marco Antonio Rodriguez kutolegeza kamba dhidi ya wenyeji hao kutokana na nyendo zao .Timu hizo zitafungua kampeini yao katika mechi ya kwanza ya nusu fainali huko Belo Horizonte.Matumaini ya wenyeji kutwaa ubingwa wa dunia yameimarika baada ya timu hiyo kufuzu kwa nusu fainali .
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Brazil iliwalaza Ujerumani  2-0 mwaka wa 2002 katika kombe la dunia huko Japan.Ujerumani Ilifuzu kwa nusu fainali hiyo baada ya kusajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa katika mechi ya robo fainali.Mechi kati ya Brazil na Ujerumani iitakaragazwa hii leo mwendo wa saa tano usiku katika uga wa Mineirao jijini Belo Horizonte


 Said PiePie,Nairobi.