Friday 11 May 2018

HULLCITY KUKICHAPA NA KOGALO WIKENDI HII

        Mabingwa wa ligi ya kandanda humu nchini  Gor Mahia watakabiliana na klabu ya Uingereza Hull City jijini Nairobi wikendi hii.
Hull city katika mechi yao ya awali
          Hull City, ambayo hushiriki katika ligi ya daraja la pili EFL nchini Uingereza wanatarajiwa kuwasili hii leo Ijumaa kwa mechi ya kirafiki siku ya Jumapiliugani  Kasarani..
Ziara ya klabu hiyo barani Afrika inafadhiliwa na kampuni ya Kamare ya Sportpesa kutoka kenya ambayo ni mfadhili wa timu tatu.

Wednesday 29 October 2014

PAUNI 500 KWA MO HAWK YA BALOTELI

           
Mario Baloteli kwenye ikifanyolewa mtindo wa Mo Hawk

M
shambuliaji wa klabu cha Liverpool mario baloteli hutumia pauni 500 kila wiki ambazo ni sawa na sh72,000(£500) kila wiki kujitengezea nywele.imeripotiwa zinasema kuwa mchezaji huyo ambaye hupendelea kunyoa mtindo wa mo hawk mbali na kubadilisha rangi ya nywele zake humlipa kinyozi wake ili kumtembelea nyumbani kwake mara tano kwa wiki.Duru zimeliambia gazeti la the sun nchini uingereza kwamba Mario huwa mkarimu sana kwani yeye hulipa pauni hamsini sawa na shilingi 7200 pesa
  kenya kila anaponyolewa.


Friday 8 August 2014

XAVI ATUNDIKA DALUGA UKUTANI


Xavi Hernandez ambaye amestaafu kwa sasa

 Kiungo wa Barcelona na Uhispania Xavi Hernandez mwenye umri wa miaka 34 ametangaza kustaafu  ya kimataifa.Hapo awali kiungo huyo alichezea timu yake ya Uhispania  na kutwaa ushindi na pia makombe mawili ya mabingwa wa Ulaya akiwakilisha nchi yake.Akiwa na umri wa miaka 20 alianza kung'ara baada ya kuipatia ushindi timu yake katika mechi ya 15 Novemba 2000 ambapo Uholanzi ililazwa bao1-0 dhidi ya Uhispania. Uhispania ilianza tena kiombe la dunia mwaka huu nchini Brazil kama moja ya timu maarufu na tarajiwa lakini wakatolewa nje katika hatua ya makundi baada ya kuchabangwa 5-1 na Uholanzi na kisha 2-0 dhidi ya Chile.huku hayo yakijiri Jopo la wanasheria wanaomwakilisha mshambulizi wa Barcelona na Urugua Luiz Suarez limesema linamatumaini makubwa kuwa shirikisho la soka duniani FIFA litapunguza marufuku ya miezi minne aliyopewa mshambulizi huyo baada ya kumngata Giorgio Chiellini.

Said PiePie,Nairobi.

Thursday 17 July 2014

DEMBA BA AELEKEA UTURUKI


Aliyekua Strika wa Chelsea Demba Ba


  Aliyekua Strika wa Chelsea Demba Ba amewasili Uturuki anakotarajiwa kukamilisha uhamiaji wake kutoka Chelsea hadi Besiktas kwa gharama ya £8m. Strika huyo mwenye umri wa mika 29 ameyathibitisha hayo katika mtandao wa Twitter akiwaamevalia  jezi ya Besi-ktas.Aidha.Wakati uo huo Chelsea wamejibu kwa kumshawishi Filipe Luis aihame Atletico Madrid ili ajiunge nao.Msimu uliopita Luis alishiriki mechi zaidi ya 40 na kilele ikawa Atletico kushinda La Liga kwa mara ya kwanza tangu 1996.Demba Ba amewahi kuifungia Chelsea mabao 14.

Said PiePie,Nairobi.

ARSENALI YAPANIA KUMNASA KHEDIRA


Sami Khedira aliyekua kiungo wa Real Madrid

    Klabu ya Arsenali imefikia hatua ya kumsajili kiungo wa kati  Sami Khedira.tokea Real Madrid kwa kima cha £20m.Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 ni mzawa wa Tunisia laikini kwa sasa anasakata soka ya kulipwa nchini Ujerumani kandarasi yake bado ipo kule  Santiago hadi mwaka wa 2015.Maelewana na klabu ya Arsenali wanazidi kunoga,aidha wanabunduki wamesha wasajili mhispania Alexis Sanchez ambaye hapo awali alikua akiwasakatia Barcelona.


 Said PiePie,Nairobi.

DIEGO AELEKEA CHELSEA


Diego Costa aliyekua strika wa  Atletico Madrid,
Strika wa Atletico Madrid,Diego Costa amejiunga na klabu ya Chelsea kwa kwa kandarasi ya miaka mitano kwa kima cha  £32mAidha mshambulizi huyo amekuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Chelsea baada ya Cesc Fabregas na Mario Pasalic.Costa amefungia Atletico mabao 52  msimu uliopita ambapo walishinda taji la kwanza la La Liga tangu 1996 na kufikia kuwa mabingwa wa ligi.Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho aliongeza mshambulizi matata katika kipindi hicho.Costa atajiunga na mchezaji mwenza wa kimataifa Cesc Fabregas kutokana na matokeo duni ya uhispania katika kombe la dunia ambapo walibanduliwa nje katika hatua ya kwanza ya kikundi.Wakati uo huo Costa ameonyesha furaha yake kujiunga na Chelsea akisema kuwa ataonyesha umahiri wake ulaya.

Said PiePie,Nairobi.

Wednesday 16 July 2014

GAAL AWASILI OLD TRAFORD LEO


Louis van Gaal kocha wa Manchester United
    Louis van Gaal anaingia hii leo Old Trafford  na kuannza rasmi kuwanoa Manchester United.
Aidha Meulensteen aliyefanya kazi na  Sir Alex Ferguson hapo awali amekiri kuwa itamchukuaLouis van Gaal ngavi ngumu kukiivisha kikosi cha United ambacho kimzembea kwa sasaMechi yao ya kwanza msimu ujao United watafungua pazia na klabu ya  Swansea.Man United walimaliza msimu uliopita katika nafasi ya saba jambo ambalo liliwaudhi maafisa wa klabu hiyo pamoja na mashabiki wa United dunia nzima.Hali iliyochangia kutimuliwa kwa david Moyes.Gaal aliwaongoza Uholazi kufika michuano ya semi fainali kombe la dunia nchini Brazil mwaka huu.

Said PiePie,Nairobi.

LIVERPOOL YAMSAJILI MARKOVIC


Lazar Markovic aliyekua mchezaji wa Benfica
 Klabu ya  Liverpool imemsajili  Lazar Markovic  kwa kima cha Pauni millioni 20 kutoka Benfica.Mserbia huyo aliiwezesha klabu ya Benfica kutwaa taji la Ureno msimu uliopita na anasema anamatumaini makubwa ya kuwaridhisha mashabiki na mwenye club hiyo.Katika dirisha la usajili msimu huu Liverpool wamenasa wachezaji kadhaa wakiwemo Mshambuliaji Rickie Lambert, 32 kwa pauni £4m na Adam Lallana, mwenye umri wa miaka 26, kwa pauni £25m, wote walitokea Southampton na Divorc Origi kutokea humu nchini.

Said PiePie,Nairobi.

Tuesday 15 July 2014

VIJANA WA TRANZOIA WAREJEA KUTOKA BRAZIL

   
Baadhi ya vijana wanao sakatia Trans Nzoia Youth Sports Association,

  Timu nchini wa umri usiozidi  miaka 18 ya Trans Nzoia Youth Sports Association,, kutoka nchini Kenya wamerejea nyumbani baada ya kushiriki kwenye mashindano ya wachezaji watano kila upande ya Football For Hope Festival mjini Rio De Janeiro, Brazil.Timu ya Delta Culture ya Cape Verde ilishinda mashindano hayo kwa kuilaza Sport Dans La Ville ya Ufaransa bao 1-0 mechi ya fainali.Timu  ya Cape Verde na Tysa ni baadhi ya timu nane za Afrika zilizoshiriki mashindano hayo yaliyojumuisha timu kutoka mataifa 32.Wachezaji hao, walitizama mechi ya robo-fainali kati ya Ujerumani na Ufaransa wanasema mbali na kandanda, wamejifunza mengi kuhusu maadili mema.Timu hiyo ilimaliza mechi zake zote bila kupoteza.

Said PiePie,Nairobi.

STARS KUMENYANA NA BURUNDI LEO


Kikosi cha Stars katika kambi ya mafunzo
      Timu ya taifa ya harambee stars itachuana na Burundi katika mechi ya kirafiki hii katika uga wa Nyayo.Mechi ya leo ni katika maandalizi ya michuano ya  kufuzu  AFCON 2015 mechi itakayo karagazwa huku Lesotho katika uga wa Maseru Julai 20.
Katika mchuano wa leo refarii wa katikati ya uwanja ni Ssali Mashood akisaidiwa na Bugembe Hussein na   Ngobi Balikoowa wote kutokkea nchi ya Uganda.Mechi hiyo imeratibiwa kusakatwa hii leo saa kumi na moja jioni katika uga wa Nyayo

Said PiePie,Nairobi.

Monday 14 July 2014

SCHOLARI APIGWA KALAMU


  Luis Felipe Scolari,aliyekua kocha wa Brazil
   S
hirikisho la kandanda nchini brazil limempiga kalamu kocha ya timu ya taifa hilo Luis Felipe Scolari baada ya kuandikisha matokeo duni katika kombe la dunia lililomalizika hapo jana.Brazil walizabwa 3-0 na Uholanzi  siku ya Jumamosi,hata hivyo habari rasmi itatolewa baadaye hii leo. Aidha Delfim Peixoto, mmoja wa wanalkamati wa shirikisho hilo amesema kuwa Scholkari hatasalia kuwa kocha wa timu hiyo baada ya kuonyesha mchezo duni.Scholari iliongoza Brazil mwaka wa 2002 katika michuano ya kombe la  dunia nchini Japa.Habari hizi zime chapishwa na Globo TV

Said PiePie,Nairobi.

UJERUMANI BINGWA WA KOMBE LA DUNIA 2014



Ujerumani watawazwa mabingwa wa kombe duina 2014 nchini Brazil
            Shangwe,nderemo,vifijo ziligubika anga ya uga wa Estadio Mineirao mjini Rio de Janeiro Brazil jana baada ya Vijana wa Joachim LoewUjerumani kuwalaza 1-0 Argentina na kutawazwa mabingwa wa kombe la dunia 2014.Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew  amesema ndoto ya timu kutwaa kombe la dunia ilitimia hapo  jana usiku. Mchezaji kiungo Mario Goetze-Super Mario aliingia kwenye madaftari ya  vya historia pale alipopachika goli la ushindi katika fainali za kombe la dunia, lililoipatia Ujerumani ubingwa wa dunia. Nyota huyo wa klabu ya Bayern Munich alitegua kitendawili cha ubingwa katika dakika  za nyoneza (113)  na kuinyamanzisha Argentina, huku ndoto ya Lionel Messi ya kufuata nyayo za nguli Diego Maradona ikiishia kwa kushindwa.
Ujerumani sasa imeshinda kombe la dunia mara nne, na kulifanya taifa hilo kubwa duniani kuwa nyuma tu ya Brazil yenye rekodi ya ushindi mara tano. Muda wa maamuzi wa fainali hiyo iliyojawa na msisimko na magoli yaliyofungwa kwa ustadi mkubwa ulikuja wakati timu hizo zikinyemelewa na mikwaju ya penati mbele ya watazamaji 74,738 katika uwanja maarufu wa Maracana mjini Rio de Janeiro.Mchezaji bora wa mechi hiyo ya fainali Goetze aliituliza kifuani krosi ya Andre Schuerrle na bila kufanya ajizi akasukuma mkwaju uliyomduwaza mlinda mlango wa Argentina Sergio Romero, kwa goli la ushindi lililomfanya nahodha Philip Lahm kubeba kombe la dunia.





 
Mario Gotze aadhimisha bao lak
Ujerumani ambayo iliinyeshea Brazil mvua ya magoli 7 -1 katika mchezo wa nusu fainali, imekuwa timu ya kwanza ya Ulaya kubeba kombe la dunia katika Amerika ya Kusini. Walianza kushinda taji hilo mwaka 1954, na kulirudia mwaka 1974 na 1990. Wamekuwa wakilikosakosa ama kwa kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali au fainali katika miaka ya hivi karibuni.Lionel Messi hakucheza kama alivyotarajiwa. Kiungo wa kati Javier Mascherano alisema ni vigumu kueleza, kwani walifanya kila kitu kushinda na walikuwa na nafasi nzuri zaidi.Aidha Messi, Gonzalo Higuain na Rodrigo Palacio walikosa nafasi nzuri cha juu wakati kichwa cha Benedikt Hoewedes kiligonga mwamba kwa upande wa Ujerumani mbele ya maelfu ya mashabiki wakiwemo rais wa Ujerumani Joachim Gauck, Kansela Angela Merkel, rais wa Urusi Vladmir Putin na mwenyeji wao rais wa Brazil Dilma Roussef.




 
Mbwembwe za mashabiki wa Ujerumani
Wakiwa wamebeba kombe mikononi mwao, wachezaji wa Ujerumani waliimba pamoja na mashabiki wao, wimbo maarufu wa Am Tag Wie Diesen (Katika siku kama hii) uliyopigwa na bendi ya Ujerumani ya Die Toten Hosen na kuchezwa uwanjani. Ilikuwa ndoto iliyotimia baada ya subira ya miaka mingi.Kufuatia ushindi huo Ujerumani walinyakua taji la nne la dunia.Kipa wa Ujerumani Manuel Nuer alitawazwa kuwa kipa bora na akatuzwa ''Golden Glove''.Rais wa Urusi Vlamir Putin alipokea ithibati rasmi ya kuandaa makala yajayo ya kombe la dunia kutoka kwa rais wa FIFA.Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwepo Maracana kwa mualiko wa rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa Brazil Dilma Rousseff. Makala yajayo ya kombe la dunia yataandaliwa nchini Urusi mwaka wa 2018.



Said PiePie,Nairobi.