 |
Lukas Podolski Strika wa Ujerumani |
Lukas Podolski hatashiriki mchuano wa kufuzu katika robo fainali dhidi ya
Algeria utakaochezwa hii leo.Kocha wa Ujerumani Joachim Löw amewadokezea
waandishi habari katika kambi ya mafunzo ya Ujerumani ya Santo Andre kuwa
Podolski hatakuwa tayari kwa wakati unaofaa kucheza mpambano wa Algeria,
akisema kuwa mchezaji huyo wa pembeni wa Arsenal atastahili kupumzika kwa siku
mbili au tatu.Beki Jerome Boateng amepata jeraha
jingine, mara hii akiumia katika goti lake la kushoto. Löw amesema jeraha hilo
siyo ba ya sana.Dhidi ya Algeria, Ujerumani
inapambana na timu dhabiti zaidi ya Afrika katika dimba hilo kufikia sasa. Löw
amesema Desert Warriors ni hatari mno na wenye nguvu uwanjani na hivyo
haitakuwa kazi rahisi kwa vijana wake, hata hivyo ameongeza kuwa timu yake inaweza kuimarika
baada ya kutoka sare na Ghana na kuwapiku kwa ushindi mdogo sana timu ya
Marekani yake Jürgen Klinsmann katika hatua ya makundi.
Said PiePie,Nairobi