Divorc Origi,anayesakatia kabumbu Ubelgiji na Lille ya Ufaransa
Mjombake Divorc Origi, Austin Oduor,
amesema strika huyo wa taifa ya Ubelgiji anapania kuelekea Uingerza
msimu ujao.Aidha Oduor, ameongeza kuwa strika
yuko katika hali nzuri ya kuelekea Uingereza msimu ujao.Origi, mwenye umri wa miaka 19
ameonyesha mchezo mzuri kwenye mashindano ya kandanda ya kombe la dunia nchini
Brazil, na kwa mara ya kwanza alicheza dakika zote tisini dhidi ya Marekani
kwenye mechi yao ya raundi ya pili, na hatimaye Romelu Lukaku akaingia uwanjani
naye Origi akapumzika.Miongoni mwa timu za ligi kuu ambazo
zinammezea Origi mate ni Liverpool,
Tottenham Hotspurs na Arsenal lakini kuna dalili Liverpool itamnasa kinda huyo
ambaye alizaliwa Ubelgiji wakati babake Mike Okoth, raia wa Kenya, alipokuwa
akicheza kandanda ya kulipwa nchini humo.Origi mwenyewe anasema ana hamu sana
ya kushiriki ligi kuu ya England bora apate klabu kitakachomfurahisha.Babake Origi ni shabiki sugu wa
Liverpool hivyo basi huenda akamshawishi mwanawe ajiunge na bingwa hao mara 18
wa ligi kuu ya England.Lakini kabla mashindano ya kombe la
dunia yaanze Okoth alisema atampa Origi uhuru wa kuamua ni klabu kipi anataka
kuchezea England endapo atagura Lille ya Ufaransa.