![]() |
Mashabiki hakiki wa timu ya taifa ya Algeria almaarufu Desert folks |
Mashabiki wa timu ya taifa ya Algeria waliandaa serehe babubkubwa baada ya timu yao kufuzu kwa michuano ya mchujo
ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.Algeria ilifuzu katika awamu hiyo ya pili nchini
Brazil baada ya kupata sara ya bao moja kwa moja na Urusi ambao
waliobanduliwa katika michuano hiyo.Fataki ziliwashwa usiku kucha katika mji mkuu wa Algeria, Algiers huku makundi ya raia wakicheza densi na kupeperusha bendera.
Misafara ya magari ilipitia katika maeneo mengi
ya mji mkuu Algiers huku barabara huku shangwe,nderemo na vifijo vikimiliki anga.Katika raundi ya pili, timu ya Algeria itakabana koo na Ujerumani siku ya jumatatu.Katika michuano ya kombe la dunia mnamo mwaka
1982,Ujerumani ilishtumiwa kwa kucheza sare na Austria
kimakusudi ili kuhakikisha kuwa timu zote mbili zinafuzu ili kuiondoa
Algeria.Said PiePie,Nairobi