 |
Edinson Cavani anayesakatia Uruguay na Paris Saint-Germain |
Katika dimba la Kombe la Dunia, Uingereza wanashikilia mkia kwa kundi lao
baada ya kuzamishwa na Uruguay kwa kufungwa 2-1.
Luis Suarez ndiye aliyeiangamiza Uingereza kwa kuyafunga magoli yote mawili
wakati Wayne Roney akiifungia Uingereza goli la kufutia machozi na ambalo
ndilo lake la kwanza katika Kombe la Dunia. Kwingineko, Colombia wamefuzu
katika awamu ya 16 baada ya kuwabwaga Cote d'Ivoire magoli mawili kwa
moja. Katika mchuano mwingine, Japan na Ugiriki zilitoka sare ya
kutofungana bao katika. Ugiriki ililazimika kucheza kwa dakika 52 bila ya
nahodha wake Kostas Katsouranis, ambaye alitimuliwa uwanjani kwa kufanya
makosa yaliyompa kadi mbili za njano. Hii leo Ijumaa, Italia watashuka
dimbani dhidi ya Costa Rica wakati Uswisi wakikabana koo na Ufaransa kabla
ya Honduras kuangushana na Equador.
Said PiePie,Nairobi.