Friday, 11 July 2014

SANCHEZ AWASILI EMIRATES


Alexis Sanchez aliyekua mchezaji wa Barcelona hapo awali

      Hatimaye klabu ya Arsenali imenasa huduma za mchezaji Alexis Sanchez kutokea klabu ya Barcelona kwa kima cha dola pauni 32.Sanchez mwenye umri wa miaka 25 ndiye mchezaji wa kwanza kusajiliwa msimu huu aidha Arsenali inapania kunasa Mathieu Debuchy kutoka klabu ya Newcastle.Wakati uo huo Sanchez ameonuesha kuridhika kwake kuhaima klabu ya Arsenali akisema anatarajia kupata tajriba ya juu n klabu hiyo.Klabu hiyo pia anammezea mate kiungo wa kati mzaliwa wa Tunisia anayeisakatia  Ujerumani Sami Khedira hata hivyo duru zinaripoti kuwa  kitita ambacho Khedira huenda akalipwa kitamfanya awe mchezaji ghali katika kambi ya wanabunduki.

Said PiePie,Nairobi.







KLOSE ATIA FORA NCHINI BRAZIL



 
Strika wa Ujeruamani Miroslav Klose
     Miroslav Klose wa  Ujeruamani ndiye mfungaji wa mabaoi mengi katika Kombe la Dunia, baada ya kufunga goli lake la 16 dhidi ya Brazil, na kuifuta rekodi ya mshambuliaji wa Brazil Ronaldo.Klose mwenye umri wa miaka 36, anacheza katika Kombe la Dunia kwa mara yake ya nne, tayari alikuwa ameifikia rekodi iliyowekwa na Ronaldo ya magoli 15 wakati alipofunga goli la kusawazisha katika mchuano waliotoka sare ya 2-2 dhidi ya Ghana katika awamu ya makundi kabla ya kufunga la 16 katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Brazil mjini Belo Horinzonte.Goli hilo lilikuwa lake la kwanza katika nusu fainali ya Kombe la Dunia na mojawapo ya mabao muhimu kwa sababu liliiweka Ujerumani kifua mbele 2-0.Klose, mwanasoka mtulivu anayechezea klabu ya Lazio baada ya kuanzia Kaiserslautern, Wrder Bremen na Bayern Munich.Kocha wake Joachim Löw amemmiminia sifa mshambuliaji huyo, akisema kikosi kizima kimefurahishwa na mafanikio ya Klose, na ni mafanikio ambayo alistahili kuyapata.

Said PiePie,Nairobi.

UJERUMANI KUMENYANA NA URGENTINA KWENYE FAINALI


Baadhi ya wachezaji wa timu ya Ujerumani kwenye kambi ya mazoezi



      Ujerumani na Argentina zitakutana kwenye mechi ya fainali ya kombe la dunia Jumapili Julai tarehe 13 mjini Rio De Janeiro.Aidha mshindi ataweka kibindoni dola milioni 35 na wa pili $25 milioni, wa tatu $22milioni wa nne $20 milioni.Timu nne zilizoondolewa kwenye robo-fainali zitapokea $14 milioni kila mmoja, timu nane zilizong'olewa raundi ya pili $9 milioni na timu 16 zilizoondolewa raundi ya kwanza $8 milioni kila mmoja.     

Mchezaji wa safu ya mbele wa Argentina Angel Di Maria
Ujerumani ilifuzu kwa awamu ya  fainali baada ya kuwalaza Brazil mabao 7-1 na Argentina ikaiondoa Uholanzi mabao 4-2 kupitia mikwaju ya penalti ktika mechi ya nusu-fainali. Kwa jumla timu 32 zimeshiriki mashindano ya mwaka huu kwenye mechi 64 na wachezaji 736 wakajitosa uwanjani.Hii ni mara ya tatu Ujerumani na Argentina wanakutana fainali ya kombe la dunia, mara ya kwanza ikiwa mwaka wa 1986 nchini Mexico Argentina ikashinda 3-2 kisha wakapatana tena mwaka wa 1990 nchini Italia na Ujerumani ikalipiza kisasi kwa kuinyoa Argentina bao 1-0.

Argentina ilifuzu baada ya kushinda Uholanzi huku Ujerumani ikiwaadhibu Brazil 7-1.


Said PiePie,Nairobi.