Saturday, 12 July 2014

GOR YAZIMA STIMA


Kikosi cha Gor kwenye mbwembwe
     Gor Mahia imeandikisha ushindi mnono hii leo baada ya kuwalaza Western Stima  2-0 katika mchuano wa ligi ya primia nchini ulio karagaziwa katika uga wa Afraha mjini Naivasha jioni ya leo. Eric Ochieng aliyekuwa mchezaji wa  Talanta FC hapo awali na Timothy Otieno waliwatia Kogalo kifua mbele kwa kufunga mabao mawili mtawalia.Gor walimiliki mpira kwa mda mrefu katika dakika za kwanza hata hivyo katika dakika ya nane Stima walivamia lango la Gor huku wakiponea kwenye tundu la sindano.
Baadhi ya wachezaji wa Western Stima
Bao la kwanza la Gor lilipatikana katika dakika ya 61 kupitia kona iliyocharazwa na   Erick Ochieng.Huku bao la pili likitiwa kimiani naTimothy Otieno.












  Aidha kocha wa Gor,Bobby Williamson amewapongeza vijana wake kwa kuonyesha mchezo mzuri uliokomaa.Refarii wa katikati ya uwanja alikua  Amos Ichingwa.Wakati uo huo Sony sugar iewalaza Tusker Fc 1-0


Said PiePie,Nairobi.

USALAMA WAIMARISHWA RIO DE JENEIRO



         
     Maafisa wa polisi  mjini Rio de Jeneiro wameanza kuweka usalama na ulinzi mkali huku masaa yakihesabuliwa fainali za kombe la dunia zing'oe nanga hapo kesho kati ya Argentina na Ujerumani Zaidi ya maafisa elfu hamsini wa polisi,maafisa wa zima moto,pamoja na majeshi yatashirikishwa katika kuimarisha ulinziRais wa Brazil Dilma Roussef anatarajiwa kuhudhuria fainali hizo katika uwanja wa Maracana akiandamana na marais wengine tisa akiwemo rais Vladmir Putin wa Urusi na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.
Meli ishirini na tano zitakuwa zinapiga doria katika pwani ya mji huo.
Huku hayo yakijiri, Ujerumani inajiandaa kushuka dimbani katika fainali ya Kombe la Dunia katika uwanja wa Maracana Brazil, dhidi ya Argentina huku ikipigiwa upatu kumzidi nguvu mpinzani wake huyo wa Amerika ya Kusini.


Kikosi chaUjerumani katika kambi ya maandalizi
Katika mechi tatu za mwisho ambazo timu hizo zimekutana, Wajerumani ndio walioibuka washindi. Ujerumani ilishinda katika fainali ya 1990 mjini Rome 2-1 na kuwa bwaga Argentina katika robo fainali za Kombe la Dunia 2006 kupitia mikwaju ya penalti  mjini Berlin, na tena ikawachabanga magoli manne kwa sifuri katika robo fainali miaka minne iliyopita mjini Cape Town, Afrika Kusini. Nayo Argentina iliipiku iliyokuwa Ujerumani ya Magharibi magoli matatu kwa mawili katika fainali ya 1986 mjini Mexico City.


Brazil inachuana na Uholanzi hii leo.AidhaLoius Van Gaal, kocha wa Uholanzi anasema mchuano huu huwa hauna maana. Mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu kwa kawaida huwa siyo maarufu, na kivumbi cha leo mjini Brasilia kitakuwa tu cha kuwaliwaza wenyeji Brazil ambao bado wana maruweruwe ya kichapo walichopewa na Ujerumani.


 Said PiePie,Nairobi.