Monday, 14 July 2014

UJERUMANI BINGWA WA KOMBE LA DUNIA 2014



Ujerumani watawazwa mabingwa wa kombe duina 2014 nchini Brazil
            Shangwe,nderemo,vifijo ziligubika anga ya uga wa Estadio Mineirao mjini Rio de Janeiro Brazil jana baada ya Vijana wa Joachim LoewUjerumani kuwalaza 1-0 Argentina na kutawazwa mabingwa wa kombe la dunia 2014.Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew  amesema ndoto ya timu kutwaa kombe la dunia ilitimia hapo  jana usiku. Mchezaji kiungo Mario Goetze-Super Mario aliingia kwenye madaftari ya  vya historia pale alipopachika goli la ushindi katika fainali za kombe la dunia, lililoipatia Ujerumani ubingwa wa dunia. Nyota huyo wa klabu ya Bayern Munich alitegua kitendawili cha ubingwa katika dakika  za nyoneza (113)  na kuinyamanzisha Argentina, huku ndoto ya Lionel Messi ya kufuata nyayo za nguli Diego Maradona ikiishia kwa kushindwa.
Ujerumani sasa imeshinda kombe la dunia mara nne, na kulifanya taifa hilo kubwa duniani kuwa nyuma tu ya Brazil yenye rekodi ya ushindi mara tano. Muda wa maamuzi wa fainali hiyo iliyojawa na msisimko na magoli yaliyofungwa kwa ustadi mkubwa ulikuja wakati timu hizo zikinyemelewa na mikwaju ya penati mbele ya watazamaji 74,738 katika uwanja maarufu wa Maracana mjini Rio de Janeiro.Mchezaji bora wa mechi hiyo ya fainali Goetze aliituliza kifuani krosi ya Andre Schuerrle na bila kufanya ajizi akasukuma mkwaju uliyomduwaza mlinda mlango wa Argentina Sergio Romero, kwa goli la ushindi lililomfanya nahodha Philip Lahm kubeba kombe la dunia.





 
Mario Gotze aadhimisha bao lak
Ujerumani ambayo iliinyeshea Brazil mvua ya magoli 7 -1 katika mchezo wa nusu fainali, imekuwa timu ya kwanza ya Ulaya kubeba kombe la dunia katika Amerika ya Kusini. Walianza kushinda taji hilo mwaka 1954, na kulirudia mwaka 1974 na 1990. Wamekuwa wakilikosakosa ama kwa kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali au fainali katika miaka ya hivi karibuni.Lionel Messi hakucheza kama alivyotarajiwa. Kiungo wa kati Javier Mascherano alisema ni vigumu kueleza, kwani walifanya kila kitu kushinda na walikuwa na nafasi nzuri zaidi.Aidha Messi, Gonzalo Higuain na Rodrigo Palacio walikosa nafasi nzuri cha juu wakati kichwa cha Benedikt Hoewedes kiligonga mwamba kwa upande wa Ujerumani mbele ya maelfu ya mashabiki wakiwemo rais wa Ujerumani Joachim Gauck, Kansela Angela Merkel, rais wa Urusi Vladmir Putin na mwenyeji wao rais wa Brazil Dilma Roussef.




 
Mbwembwe za mashabiki wa Ujerumani
Wakiwa wamebeba kombe mikononi mwao, wachezaji wa Ujerumani waliimba pamoja na mashabiki wao, wimbo maarufu wa Am Tag Wie Diesen (Katika siku kama hii) uliyopigwa na bendi ya Ujerumani ya Die Toten Hosen na kuchezwa uwanjani. Ilikuwa ndoto iliyotimia baada ya subira ya miaka mingi.Kufuatia ushindi huo Ujerumani walinyakua taji la nne la dunia.Kipa wa Ujerumani Manuel Nuer alitawazwa kuwa kipa bora na akatuzwa ''Golden Glove''.Rais wa Urusi Vlamir Putin alipokea ithibati rasmi ya kuandaa makala yajayo ya kombe la dunia kutoka kwa rais wa FIFA.Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwepo Maracana kwa mualiko wa rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa Brazil Dilma Rousseff. Makala yajayo ya kombe la dunia yataandaliwa nchini Urusi mwaka wa 2018.



Said PiePie,Nairobi.

No comments:

Post a Comment