Friday, 13 June 2014

MIENO AHAMIA INGWE


 


 
Humphrey Mieno  aliyekua mchezaji wa Sofapaka

         Ni rasmi kuwa Humphrey Mieno amejiunga na kikosi cha AFC Leopards baada ya kugura timu ya  Sofapaka almaarufu Batoto Ba Mungu kwa kandarasi ya miaka miwili.Wanamvinyo Tusker Fc pia walikua wakimmezea mate lakini Ingwe wakaonyesha ukali wamakucha baada ya kumnyakua haraka.Rais wa Sofapaka Elly Kalekwa amesema kuwa  uhamisho huo ulifanywa hapo jana.Uhamisho huo uliendeshwa na shirika la International Sports and Entertainment Management Limited (ISEML).

Said PiePie,Nairobi.

UHURU AFADHILI STARS KUELEKEA BRAZIL



Rais Kenyatta akiwa na kikosi cha Harambee Stars
         Rais  Uhuru Kenyatta amekifadhili kikosi cha Harambe Stars kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la duniaHafla hiyo,ilifanyika katika ikulu ya Rais ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa vyeti vya usafiri kwenda Brazil.
Kenyatta na mkewe  Margaret Kenyatta wamekifadhili kikosi hicho dola elfu 40. Aidha Rais amesema lengo lake hasa ni kuwapa matumaini na motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka nchini Kenya.Rais  hakwenda na kikosi hicho bali aliwahauri wachezaji hao kuwa mabalozi wema wa Kenya nchini Brazil.Ufadhili huo unawadia miezi sita baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara wa kocha wa timu hiyo kwa miakja miotano ijayo.
Kenya haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia lakini ziara hii kwa vijana wa Harambee Stars itawafungua macho huku wakiwa na azma ya kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili na kujiandaa kuchuana na Lesotho tarehe 18 mwezi ujao.Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji ; Clifton Miheso, David Owino, Joackins Atudo, Abud Omar, James Situma, Wilson Obungu, Allan Wanga, Jacob Keli, Edwin Lavatsa, Francis Kahata, Joe Muiruri Gachoka, Jerim Onyango, Musa Mohammed, Hillary Kimaru Kipchillat, Samuel Njenga Miringu, Duncan Ochieng’, Dennis Oliech, Paul Mungai,
Wakiwemo maafisa wa usimamizi na kocha  Adel Amrouche, James Nandwa, Jacob Ghost Mulee, Kennedy Odhiambo, Elly Mukolwe, Daniel Francis Irukan, Julius Maina Kigaga.

Said PiePie,Nairobi

MWANAMICHEZO: BRAZIL WAILAZA KROATIA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI

MWANAMICHEZO: BRAZIL WAILAZA KROATIA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI: Uga wa Corithians Sao Paulo unachukua mashabiki 61,500     

Sherehe za Ufunguzi wa Kombe la Dunia Brazil 2014 ziliaanza  ...

BRAZIL WAILAZA KROATIA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI


   
 
Uga wa Corithians Sao Paulo unachukua mashabiki 61,500
     Sherehe za Ufunguzi wa Kombe la Dunia Brazil 2014 ziliaanza  kwa mbwembwe ya aina yake huku  mwimbaji wa kimataifa Jinnifer Lopez akipamba jukwaa Katika uga  wa Corithians Sao Paolo.Timu ya taifa la Croatia iliwachezesha : Pletikosa; Srna, Ćorluka, Lovren, Vrsaljko; Modrić, Rakitić, Perišić, Brozović; Olić, Jelavić huku nao wapinzani wao Brazil wakiwashirikisha katika kikosi chao : Cesar; D.Alves, T.Silva, D.Luiz, Marcelo; Paulinho, L.Gustavo; Hulk, Oscar, Neymar; Fred. 





Marcelo Vieira  anayeichezea Real Madrid
Mercelo alijifunga katika kipindi cah kwanza na kuipa Croatia bao la kwanza .
Neymar aliifungia bao la kwanza na  pili Brazil kupitia kwa mkwaju wa penalti hata hivo maswali yanazidi kuibuka  kuhusiana na penalti hiyo.Mchezaji huyo  aliiandikisha rekodi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya Njano kwa kumpiga kumbo Modric katika mechi za kombe la dunia mwaka huu.Katika dakika ya 47 Neymar alifanyiwa badiliko huku mchezaji Ramires anayeisakatia Chelsea akijaza pengo lake.Oscar amhakikishia kocha Luiz Felipe Scolari ushindi muhimu katika mechi ya ufunguzi wa dhidi ya Croatia kwa kupachika kimiani bao la tatu na la ushindi.
Kocha wa Croatia Niko Kovac ambaye alikuwa na hasira amesema mwamuzi kutoka Japan Yuichi Nishimura aliyesimamia pambano hilo la jana alikuwa hayuko katika kiwango chake, baada ya kutoa penalti kwa Brazil ambayo imebishaniwa na kubadilisha kabisa mwelekeo wa mchezo huo wa ufunguzi.
Croatia wako katika nafasi ya 18 ya orodha ya FIFA ya timu bora duniani , ilikuwa ikijaribu kuzuwia na kuwatuliza Brazil katika kipindi cha pili hadi pale refa Yuichi Nishimura alipoamua upigwe mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wa Brazil Fred kuanguka wakati akipambana na mlinzi wa Croatia Dejean Lovren
Hii  leo Simba wa Nyika , Cameroon , wataingia uwanjani kupambana na Mexico katika mchezo mwingine wa kundi A, wakati mabingwa watetezi Uhispania inaanza kampeni ya kurelijesha taji hilo mjini Madrid kwa kupambana na Uholanzi katika mchezo wa kundi B.

Said PiePie,Nairobi.