Tuesday, 1 July 2014

"RAMADHAN HAIKUTUADHIRI" ALGERIA WAKIRI.


 
Mlindalango wa Algeria Rais M’Bolh
      Rais M’Bolhi golkipa wa Algeria amekanusha madai wachezahi wao walishindwa na Ujerumani kutokana na wao kuwa wadhaifu kwa kufunga saumu.M’Bolhi ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo ambayo Algeria walishindwa mabao 2-1 na Ujerumani katika muda wa ziada anasisitiza kuwa Saumu hakikuchangia kwao Kushindwa.Aidha M’Bolhi anasema kuwa wachezaji hao wamekwisha zoea kucheza hata wakiwa kwenye mfungo na hivyo haipaswi kutolewa kama sababu .Kabla ya mechi hiyo kulikuwa na ubishi baada ya kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic kukataa kuulizwa maswali kuhusiana na mfungo wa Ramadhan ambao ulikuwa umeanza jumamosi .Halilhodzic alikataa kufichua idadi ya wachezaji wake ambao wanafunga mfungo wa Ramadhan kabla ya mechi .Wakati uo huo kocha huyo alikataa kujibu swali ikiwa wachezaji wake watafunga Ramadhan au la wakati wakicheza.Kulingana na dini ya Kislamu ,Ramadhan ni nguzo muhimu ya dini na ifikapo wakati huo kila mtu mwenye umri wa baleghe hujinyima chakula kuanzia alfajiri hadi magharibi .Hiyo inaamisha kuwa wachezaji wa Algeria hawakuwa wamekula chochote hadi baada ya kipindi cha pili cha mechi hiyo ndipo waliporuhusiwa  kunywa na  kula .Ujerumani ilifuzu kwa robo fainali ya kombe la dunia ambapo watakutana na Ufaransa ijumaa ijayo.

Said PiePie,Nairobi.

KOCHA WA NIGERIA AFUNGANYA VIRAGO



Aliyekua kocha wa Nigeria almaarufu Super Eagles  Stephen Keshi 
      Stephen Keshi  Kocha wa Nigeria amejiuzulu baada ya timu ya Super Eagles kuondolewa kutoka kwenye kipute cha kombe la dunia walipozabwa 2-0 na Ufaransa .Keshi mwenye umri wa miaka 52 alichukua wadhfa huo mwaka wa 2011 na akaiongoza timu hiyo na kutwaa ubingwa wa afrika mwaka uliopita .Wakati uo huo nahodha wa timu hiyo Joseph Yobo aliyejifunga bao la pili la Ufaransa naye pia ametangaza kustaafu .Keshi chini ya uongozi wake Super Eagles imefuzu kwa mara ya kwanza katika mkondo wa pili wa kombe la dunia tangu mwaka wa 1998 licha ya kukumbwa na migomo ya wachezaji wake wakidai malimbikizi ya marupurupu.kocha waliojiuzulu kufuatia matokeo duni katika kombe la dunia kutimia makocha 6.Hadi sasa kocha wengine waliojiuzilu ni pamoja na Luis Suarez, wa Honduras, Carlos Queiroz wa Iran's ,Alberto Zaccheroni wa Japan , Cesare Prandelli wa italia na Sabri Lamouchi wa Ivory Coast.Hapo awali Keshi, aliwahi kuhudumu kama kocha wa Mali na Togo.

Said PiePie,Nairobi.

KRA YASAJILI 4


Kocha wa KRA Ken Kenyatta akitoa maelekezo

    Watoza ushuru  (KRA)  wamewasajili wachezaji wa nne akiwemo  Hassan Musaja Mohammed aliyekua kwa kikosi cha AFC Leopards  kwa kandarasi ya miezi sita,Ezekiel Odero tokea  Thika United  na pia aliyekua mchezaji wa  Tusker FC na  Sofapaka hapo awali George Opiyo. Anayekamilisha orodha hii ni Robert Binja aliyekua strika wa Sofapaka wali.

Said PiePie,Nairobi.

WANGA AELEKEA SUDAN KWA MKOPO

Aliyekua mchezaji wa Afc leopards Allan Wetende Wanga

      Wakenya nchini Sudan wamempokea  aliyekua strika wa AFC leopards Allan Wanga kwa shanngwe na nderemo  baada yake kujiunga na kikosi cha El Merreikh kwa kandarasi ya mwaka mmoja.Pamoja na waliompokea Wanga ni wachezaji  wa El Merrieh na Suleiman Akida mwanakamati wa timu hiyo. Kiungo wakati wa Gor Mahia  Teddy Akumu pia anasakatia klabu hiyo

Said PiePie,Nairobi.