John Brooks liliwapa Marekani
ushindi uliotokana na kibarua kigumu wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Ghana
katika uwanja wa Estadio das Nunas mjini Natal
Clint Dempsey alifunga goli la kasi
sana na ambalo ni la tano katika historia ya Kombe la Dunia, na kuwaweka kifua
mbele vijana wa kocha Jurgen Klinsmann baada ya sekunde 29.
Andre Ayew aliwapa
pointi 1 Ghana almaarufu Black Stars alipofunga bao safi baada ya
kuandaliwa pasi kisigino na Asamoah Gyan, wakati kukiwa kumesalia
dakika 8 katika kipindi cha kwanza
Uzembe wa Ghana ulimpa fursa beki wa
Marekani Brooks kufunga kichwa safi kutokana na mkwaju wa kona zikiwa zimesalia
dakika 5 mpira kumalizika. Hilo lilikuwa goli lake la kwanza la kimataifa, na
likampa ushindi Jurgen Klinsmann ambaye ameadhimisha mchuano wa 50 akiwa na
timu ya taifa ya Marekani.
 |
Shabiki wa Ghana na mbwembwe zake |
Black Stars walitawala mchezo kwa
muda mrefu lakini mwishoni walijuta kwa kushindwa kuzitumia fursa zao
kufunga mabao.Marekani sasa itacheza mchuano ujao
dhidi ya Ureno, ambao walizabwa magoli 4-0 na Ujerumani, wakiwa na matumaini
kuwa wanaweza kufuzu katika 16 za mwisho.
Kocha Klinsmann amesema “kuna mambo
ambayo tunaweza kuimarisha lakini leo tumepata points tatu tulizozihitaji
sana”. Aliongeza kuwa “Ghana ni timu nzuri na wanajua namna ya kuumiliki
mchezo. Hilo lilitarajiwa”.
Kocha wa Ghana Kwesi Appiah alikanusha
madai kuwa mchezo wa vijana wake ulitokana na mgomo baridi wa wachezaji lakini
akakiri kuwa Black Stars bado wasubiri malipo yao kamili ya marupurupu.
Ghana walifika katika robo fainali
ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka wa 2010, sasa wanakabiliwa na
mlima mkubwa wa kuukwea ili kujiondoa katika kundi hilo ambalo lina Ujerumani,
Ureno.
Marekani
imelipiza kisasi cha kushindwa katika michuano miwili ya kombe la dunia na
Ghana .
Said Piepie,Nairobi.