![]() |
Kikosi cha Leopards alamaarufu Ingwe |
Timu ya AFC Leopards imefutilia mbali uhamisho wa wachezaji wake iliokuwa imepania kuwasajili kwa mkopo,miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na Strika Dennis Dodi, Duncan Otieno na Sadiq Mohammed.Kulingana na katibu wa Ingwe Timothy Lilumbi amesema kuwa maelewano na klabu mbalimbali hayajaafikiwa.Leopards ilikua inapania kusajili wachezaji katika klabu ya Kakamega Homeboyz, Thika United na Mathare United.
Said PiePie,Nairobi.