Monday, 30 June 2014

PODOSKI KUKOSA MECHI DHIDI YA ALJERIA



Lukas Podolski Strika wa Ujerumani
     Lukas Podolski hatashiriki  mchuano wa kufuzu katika robo fainali dhidi ya Algeria utakaochezwa hii leo.Kocha wa Ujerumani Joachim Löw amewadokezea waandishi habari katika kambi ya mafunzo ya Ujerumani ya Santo Andre kuwa Podolski hatakuwa tayari kwa wakati unaofaa kucheza mpambano wa Algeria, akisema kuwa mchezaji huyo wa pembeni wa Arsenal atastahili kupumzika kwa siku mbili au tatu.Beki Jerome Boateng amepata jeraha jingine, mara hii akiumia katika goti lake la kushoto. Löw amesema jeraha hilo siyo ba ya sana.Dhidi ya Algeria, Ujerumani inapambana na timu dhabiti zaidi ya Afrika katika dimba hilo kufikia sasa. Löw amesema Desert Warriors ni hatari mno na wenye nguvu uwanjani na hivyo haitakuwa kazi rahisi kwa vijana wake, hata hivyo  ameongeza kuwa timu yake inaweza kuimarika baada ya kutoka sare na Ghana na kuwapiku kwa ushindi mdogo sana timu ya Marekani yake Jürgen Klinsmann katika hatua ya makundi.

Said PiePie,Nairobi


No comments:

Post a Comment