Thursday, 26 June 2014

UFARANZA KUKUTANA NA NIGERIA MKONDO WA PILI



Kikosi cha timu ya Ufarnza
         Ufaranza ilikamilisha mechi za makundi kwa sare tasa dhidi ya Ecuador.Kwa sasa Ufaransa imesalia kileleni mwa kundi E ikiwa na alama 7 moja zaidi ya Switzerland iliyoisakama Iran katika mechi ya mwisho.Nao Argentina  walifuzu katika raundi ya 16 bora ambapo sasa watachuana na Nigeria .Ufaransa itachuana na Nigeria katika mkondo wa pili wa kombe la dunia.Mechi hiyo ilishuhudia kadi nyekundu ya nane katika mashindano haya ya kombe la dunia ,nahodha wa Ecuador Antonio Valencia alipofurushwa uwanjani baada ya kumchezea vibaya Lucas Digne.Ufaransa itachuana na Nigeria katika mkondo wa pili wa kombe la dunia.Ufaransa sasa itamenyana  na Nigeria waliomaliza mechi yao ya kundi F kwa kushindwa na Argentina kwa mabao 3-2 siku ya Jumatatu tarehe 30 katika Estadio Di Nationale.Washindi wa kundi hilo Argentina watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Switzerland Jumanne ijayo katika uga wa Arena De Sao Paulo.


 Said PiePie,Nairobi.

No comments:

Post a Comment