|  | 
| Mashabiki hakiki wa timu ya taifa ya Algeria almaarufu Desert folks | 
       Mashabiki wa timu ya taifa ya  Algeria waliandaa serehe babubkubwa baada ya timu yao kufuzu kwa michuano ya mchujo 
ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.Algeria ilifuzu katika awamu hiyo ya pili nchini
 Brazil baada ya kupata sara ya bao moja kwa moja na Urusi ambao 
waliobanduliwa katika michuano hiyo.Fataki ziliwashwa usiku kucha katika mji mkuu wa Algeria, Algiers huku makundi ya raia wakicheza densi na kupeperusha bendera.
Misafara ya magari ilipitia katika maeneo mengi 
ya mji  mkuu Algiers huku barabara huku shangwe,nderemo na vifijo vikimiliki anga.Katika raundi ya pili, timu ya Algeria itakabana koo na Ujerumani siku ya jumatatu.Katika michuano ya kombe la dunia mnamo mwaka 
1982,Ujerumani ilishtumiwa kwa kucheza sare na Austria 
kimakusudi ili kuhakikisha kuwa timu zote mbili zinafuzu ili kuiondoa 
Algeria.Said PiePie,Nairobi
 
 
No comments:
Post a Comment