Strika wa Uholanzi Arjen Robben katika mechi dhidi ya Mexico
Strika wa Uholanzi Arjen Robben
amekiri kuwa hakutegwa bali alijiangusha tukio lilisababisha tim uyake kutuzwa
penaltiWakati uo huo kocha wa Mexico Miguel Herrera amemkashifu refarii wa
mechi yao na Uholanzi Pedro Proenca kwa kuipendelea Uholanzi .Robben alikunguwa
katika eneo hatari karibu na lango Uholanzi ilipokuwa imesawazisha bao moja kwa
moja na ikaisaidia Uholanzi kuibuka mshindi kwa mabao 2-1 .Penalti hiyo
ilifungwa na Jan-Klaas Huntelaar aliyeilaza kimiani Mexico ilikuwa imeongoza
hadi dakika ya 88 ya kipindi cha pili kabla Wesley Sneijder kuisawazishia
Uholanzi kabla ya Huntelaar kufunga penalti iliyozua ubishi mkubwa.Herrera
alisema kuwa haikufaa refarii kutoka ulaya alipewa mechi kati ya timu kutoka
ulaya na Marekani ya kusini.Kwa sasa wapenzi wa soka duniani wanasubiri uamuzi
wa FIFA kufuatia habari zaRobben.
No comments:
Post a Comment