Thursday, 26 June 2014

SUAREZ NJE MIEZI 4

Luiz Suarez strika wa Uruguay
    Luis Suarez amepigwa marufuku ya mechi tisa na shirikisho FIFA baada ya kupatikana na kosa la kumng'ta Giorgio Chiellini kwenye mechi yao ya kombe la dunia nchni Brazil.Suarez pia  hatajihusisha na shughuli za kandanda kwa miezi minne na kutozwa faini ya dola elfu mia moja.Kutokana na adhabu hiyo Suarez sasa hatashiriki tena kwenye mechi zilizosalia za kombe la dunia.Kutokana na adhabu hiyo iliyochukuliwa na kamati ya nidhamu ya Fifa Suarez sasa hatashiriki kwenye mechi ya raundi ya pili kati ya Uruguay na Columbia Juni tarehe 28.
Adhabu hiyo pia inamaanisha Suarez hatashiriki kwenye mechi za Uruguay zijazo za kombe la dunia endapo timu itazidi kusonga mbele na zile zijazo za kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia.
Kamati hiyo ya nidhamu ya Fifa imesema Suarez hatakiwi kuingia kwenye uwanja wowote Uruguay inapocheza wakati wa adhabu hiyo ya kutocheza mechi tisa za kimataifa.Ripoti hii imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Fifa Claudio Sulser .Aidha Kamati ya Fifa imetilia maanani kila kitu kwenye kitendo hicho kabla ya uamuzi huo.Mashabiki wengi duniani wamemshutumu vikali Suarez kwa kumng'ata mchezaji huyo wa Italia kwani hii ni mara ya tatu anapatikana na hatia hiyo.

Said PiePie,Nairobi.

No comments:

Post a Comment