Friday, 11 July 2014

KLOSE ATIA FORA NCHINI BRAZIL



 
Strika wa Ujeruamani Miroslav Klose
     Miroslav Klose wa  Ujeruamani ndiye mfungaji wa mabaoi mengi katika Kombe la Dunia, baada ya kufunga goli lake la 16 dhidi ya Brazil, na kuifuta rekodi ya mshambuliaji wa Brazil Ronaldo.Klose mwenye umri wa miaka 36, anacheza katika Kombe la Dunia kwa mara yake ya nne, tayari alikuwa ameifikia rekodi iliyowekwa na Ronaldo ya magoli 15 wakati alipofunga goli la kusawazisha katika mchuano waliotoka sare ya 2-2 dhidi ya Ghana katika awamu ya makundi kabla ya kufunga la 16 katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Brazil mjini Belo Horinzonte.Goli hilo lilikuwa lake la kwanza katika nusu fainali ya Kombe la Dunia na mojawapo ya mabao muhimu kwa sababu liliiweka Ujerumani kifua mbele 2-0.Klose, mwanasoka mtulivu anayechezea klabu ya Lazio baada ya kuanzia Kaiserslautern, Wrder Bremen na Bayern Munich.Kocha wake Joachim Löw amemmiminia sifa mshambuliaji huyo, akisema kikosi kizima kimefurahishwa na mafanikio ya Klose, na ni mafanikio ambayo alistahili kuyapata.

Said PiePie,Nairobi.

UJERUMANI KUMENYANA NA URGENTINA KWENYE FAINALI


Baadhi ya wachezaji wa timu ya Ujerumani kwenye kambi ya mazoezi



      Ujerumani na Argentina zitakutana kwenye mechi ya fainali ya kombe la dunia Jumapili Julai tarehe 13 mjini Rio De Janeiro.Aidha mshindi ataweka kibindoni dola milioni 35 na wa pili $25 milioni, wa tatu $22milioni wa nne $20 milioni.Timu nne zilizoondolewa kwenye robo-fainali zitapokea $14 milioni kila mmoja, timu nane zilizong'olewa raundi ya pili $9 milioni na timu 16 zilizoondolewa raundi ya kwanza $8 milioni kila mmoja.     

Mchezaji wa safu ya mbele wa Argentina Angel Di Maria
Ujerumani ilifuzu kwa awamu ya  fainali baada ya kuwalaza Brazil mabao 7-1 na Argentina ikaiondoa Uholanzi mabao 4-2 kupitia mikwaju ya penalti ktika mechi ya nusu-fainali. Kwa jumla timu 32 zimeshiriki mashindano ya mwaka huu kwenye mechi 64 na wachezaji 736 wakajitosa uwanjani.Hii ni mara ya tatu Ujerumani na Argentina wanakutana fainali ya kombe la dunia, mara ya kwanza ikiwa mwaka wa 1986 nchini Mexico Argentina ikashinda 3-2 kisha wakapatana tena mwaka wa 1990 nchini Italia na Ujerumani ikalipiza kisasi kwa kuinyoa Argentina bao 1-0.

Argentina ilifuzu baada ya kushinda Uholanzi huku Ujerumani ikiwaadhibu Brazil 7-1.


Said PiePie,Nairobi.

Wednesday, 9 July 2014

BRAZIL WAANGAMIZWA NA WAJERUMANI



     
David Luiz ashangaa baada ya kulazwa na Ujerumani
     Mchecheto wa timu ya Brazil kunyakua Kombe la Dunia mwaka huu ulizimwa hapo jana baada ya Ujerumani kuwarindima  mabao 7-1 katika uwanja wa Estadio Mineirao ulioko Belo Horizonte.
 Hicho ndicho kilikuwa kichapo kikubwa kuwahi kutokea  katika historia yao ya miaka 100 ya soka.
Kocha Luiz Felipe Scolari aliyeonekana kupatwa na mshangao mkubwa,amewaomba mashabiki wamsamehe  kutokana na makosa waliyofanya. Rais Dilma Roussef pia alituma ujumbe wa kuituliza mioyo ya mashabiki.Thomas Müller ambaye alifunga goli lake la tano katika dimba hili, alisema hawakuamini matokeo hayo ya kushangaza. Tikiti ya Ujerumani kuelekea mjini Rio ilipatikana baada ya kipindi cha kwanza cha maangamizi ambacho walifunga magoli manne katika dakika sita.
 Thomas Müller alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 11 kutokana na mkwaju wa kona. Miroslav Klose kisha akatia kimyani la pili katika dakika ya 23 ambalo lilikuwa lake la 16 na kumfanya kuwa mfungaji wa magoli mengi katika historia ya Kombe la Dunia.


Kilio cha mashabiki wa timu ya Brazil hakikuzulika
Mashabiki wa Brazil hawakuamini macho yao namna timu yao ilivyokalifishwa uwanjani kutoka mwanzo.Toni Kroos alifunga  katika dakika ya 24 na 26 mtawalia ili kufanya mambo kuwa 4-0 na kisha Sami Khedira akabusu wavu na kufikisha 5-0 katika dakika ya 29.Goli la dakika ya mwisho lake Oscar la kufutia machozi hata halikuwatikisa mashabiki wa Brazil ndani ya uwanja. Kocha wa Ujerumani Joachim Löw amesema Brazil walishtuka baada ya kufunwga magoli ya mapema, kwa sababu hawakutarajia hilo. Hawakujua wafanye nini. Safu yao ya ulinzi haikuwa imejipanga. Ujerumani sasa wanajiandaa kwa fainali itakayochezwa katika uwanja wa Maracana Jumapili tarehe 13. Na mpinzani wao atajulikana hiii leo, kati ya Argentina na Uholanzi ambao wanakutana katika nusu fainali ya pili.



Said PiePie,Nairobi.









Tuesday, 8 July 2014

BRAZIL KUMENYANA NA UJERUMANI KWENYE NUSU FAINALI

    
Kikosi cha Brazil kikinoa makali
      M
linzi  wa Brazil Thiago Silva hatocheza katika mechi ya kwanza ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani Jumanne.Licha ya  juhudi za shirika la soka la Brazil kukata rufaa kwa shirikisho la soka duniani FIFA kutaka kadi ya pili ya njano iliyompelekea kupigwa marufuku mechi hiyo muhimu kuambulia patupu.Fifa imepuzilia mbali ombi la BFA la kuitaka ibatilishe kadi ya njano ambayo imemlazimu kocha Luiz Felipe Scolari kutafuta mlinzi mbadala kuziba pengo la nahodha huyo.
Thiago alionyeshwa kadi yake ya pili timu hiyo ilipoilaza Colombia Ijumaa iliyopita.
wakati uo huo Brazil wamepata pigo kwani Mshambuli machachari Neymar ambaye alijeruhiwa      uti wa mgongo.Kocha wa Brazil Scolari anapanga kutumia Willian kuziba pengo la Neymar.Scolari amesema kuwa Brazil itajitahidi dhidi ya Ujerumani licha ya kumkosa Neymar ambaye alikuwa ameifungia mabao manne.Aidha  kocha wa Ujerumani Joachim Low amesema kuwa Samba boys ni wakakamavu na wana jituma katika safu zao mbalimbali.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Ujerumani


 Low amemtaka refarii wa Mexico Marco Antonio Rodriguez kutolegeza kamba dhidi ya wenyeji hao kutokana na nyendo zao .Timu hizo zitafungua kampeini yao katika mechi ya kwanza ya nusu fainali huko Belo Horizonte.Matumaini ya wenyeji kutwaa ubingwa wa dunia yameimarika baada ya timu hiyo kufuzu kwa nusu fainali .
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Brazil iliwalaza Ujerumani  2-0 mwaka wa 2002 katika kombe la dunia huko Japan.Ujerumani Ilifuzu kwa nusu fainali hiyo baada ya kusajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa katika mechi ya robo fainali.Mechi kati ya Brazil na Ujerumani iitakaragazwa hii leo mwendo wa saa tano usiku katika uga wa Mineirao jijini Belo Horizonte


 Said PiePie,Nairobi.

Monday, 7 July 2014

KOCHA WA ALGERIA AFUNGANYA VIRAGO


Aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Algeria Vahid Halilhodzic
    Timu ya taifa ya  algeria imepatwa na pigo baadaya kocha wake kuijuzulu,Vahid Halilhodzic amejiuzulu licha ya ombi la kibinafsi kutoka kwa rais Abdelaziz Bouteflika akimsihi asijiuzulu.Vahid amekuwa Kocha wa Desert Folks kwa miaka mitatu.Vahid ni mzaliwa wa nchi ya Bosnia alielekeza timu hiyo katika michuano mbalimbali. Timu yake ilikuwa imesalia kati ya timu zingine 16 bora katika kitengo hicho cha ligi ya kombe la dunia.Timu ya Algeria baada ya kuilaza South Korea mabao manne kwa mawili, haikuponea mchujo baada ya kulazwa mabao mawili kwa moja dhidi ya timu ya Ujerumani.
Aidha vijana wa Vahid  walilazwa 2-1 dhidi ya Belgium, na kutoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Urusi na kufuzu kwenda raundi ya pili.


Said Piepie,Nairobi

LIVERPOOL YAMNASA ORIGI




Divock Origi anayepania kuelekea Liverpool msimu ujao
     Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema klabu yake  imekubaliana ya Lille ya Ufaransa kumsajili mshambulizi wa Ubeljiji mzaliwa wa Kenya Divock Origi kwa kima  cha pauni milioni £10m.Wakati uo huo Liverpool  inapania kumsajili kiungo cha kati wa Serbia na Benfica Lazar Markovic kwa kima cha pauni milioni £25m.Origi hata hivyo anatarajiwa kukamilisha mazungumzo juma lijalo .Aidha  Liverpool inatarajia kumuuza  Luis Suarez, kwa kwa klabu ya Barcelona kwa pauni milioni £75m.Barca imeonesha niya ya kumnunua Suarez fauka ya matatizo yaliyokumba baada ya kumngata mlinzi wa Italia Chiellini katika mechi ya kombe la dunia.Liverpool vilevile inamtaka Alexis Sanchez, katika uhamisho huo wa Suarez .Liverpool tayari imewanunua Rickie Lambert,32, kiungo Adam Lallana ,kutoka Southampton kwa gharama ya pauni ya milioni £29m.Kwa sasa Rodgers anatafuta kuimarisha kikosi chake kabla ya kushiriki mchuano wa kuwania ubingwa wa bara uropa mwakani baada ya kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita nyuma ya Man City.


Said PiePie,Nairobi





Friday, 4 July 2014

KASHFA YA VYETI GHUSHI NIGERIA


  
   
Mwenyekiti wa Shirikisho la soka nchini Nigeria,Aminu Maigari
       I
dara ya ujasusi nchini Nigeria imemtia nguvuni mwenyekiti wa shirikisho nchini humo   
Aminu Maigari  kwa madai ya vyeti ghushi.Inaripotiwa kuwa Maigari imetiwa nguvuni baada ya kuwasaili katika uwanja wa michezo wa Nnamdi Azikiwe mjini Abuja,Keshi hiyo hapo awali ilikua ikiendeshwa katika Mahakam ya Jos siku ya jumatatu.Aidha duru zinaripoti kuwa Maigari amekua akiendesha shughuli za ofisi na vyeti ghushi habari hizi pia zimetolewa na mtandao wa  www.gongnews.net

 Said PiePie,Nairobi.