| .jpg) | 
| Aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Algeria Vahid Halilhodzic | 
    Timu ya taifa ya  algeria imepatwa na pigo baadaya kocha wake kuijuzulu,Vahid Halilhodzic amejiuzulu licha 
ya ombi la kibinafsi kutoka kwa rais Abdelaziz Bouteflika akimsihi 
asijiuzulu.Vahid amekuwa Kocha wa Desert Folks kwa miaka mitatu.Vahid ni mzaliwa wa nchi ya Bosnia 
alielekeza timu hiyo katika michuano mbalimbali. Timu yake ilikuwa 
imesalia kati ya timu zingine 16 bora katika kitengo hicho cha
 ligi ya kombe la dunia.Timu ya Algeria baada ya kuilaza South Korea 
mabao manne kwa mawili, haikuponea mchujo baada ya kulazwa mabao mawili 
kwa moja dhidi ya timu ya Ujerumani.
                     
Aidha vijana wa Vahid  walilazwa 2-1 dhidi ya Belgium, 
na kutoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Urusi na kufuzu kwenda 
raundi ya pili.
Said Piepie,Nairobi
 
No comments:
Post a Comment