 |
Divock Origi anayepania kuelekea Liverpool msimu ujao |
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema klabu yake imekubaliana ya Lille ya Ufaransa kumsajili mshambulizi wa Ubeljiji mzaliwa wa Kenya Divock Origi kwa kima cha pauni milioni £10m.Wakati uo huo Liverpool inapania kumsajili kiungo cha kati wa Serbia na Benfica Lazar Markovic kwa kima cha pauni milioni £25m.Origi hata hivyo anatarajiwa kukamilisha mazungumzo juma lijalo .Aidha Liverpool inatarajia kumuuza Luis Suarez, kwa
kwa klabu ya Barcelona kwa pauni milioni £75m.Barca imeonesha niya ya kumnunua Suarez fauka ya
matatizo yaliyokumba baada ya kumngata mlinzi wa Italia Chiellini
katika mechi ya kombe la dunia.Liverpool vilevile inamtaka Alexis Sanchez, katika uhamisho huo wa Suarez .Liverpool tayari imewanunua Rickie Lambert,32, kiungo Adam Lallana ,kutoka Southampton kwa gharama ya pauni ya milioni £29m.Kwa sasa Rodgers anatafuta kuimarisha
kikosi chake kabla ya kushiriki mchuano wa kuwania ubingwa wa bara uropa
mwakani baada ya kumaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita nyuma ya
Man City.
No comments:
Post a Comment