Miroslav Klose wa Ujeruamani ndiye
mfungaji wa mabaoi mengi katika Kombe la Dunia, baada ya kufunga goli lake la
16 dhidi ya Brazil, na kuifuta rekodi ya mshambuliaji wa Brazil Ronaldo.Klose mwenye umri wa miaka 36, anacheza
katika Kombe la Dunia kwa mara yake ya nne, tayari alikuwa ameifikia rekodi
iliyowekwa na Ronaldo ya magoli 15 wakati alipofunga goli la kusawazisha katika
mchuano waliotoka sare ya 2-2 dhidi ya Ghana katika awamu ya makundi kabla ya
kufunga la 16 katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Brazil mjini Belo
Horinzonte.Goli hilo lilikuwa lake la kwanza
katika nusu fainali ya Kombe la Dunia na mojawapo ya mabao muhimu kwa sababu liliiweka
Ujerumani kifua mbele 2-0.Klose, mwanasoka mtulivu anayechezea
klabu ya Lazio baada ya kuanzia Kaiserslautern, Wrder Bremen na Bayern Munich.Kocha wake Joachim Löw amemmiminia
sifa mshambuliaji huyo, akisema kikosi kizima kimefurahishwa na mafanikio ya
Klose, na ni mafanikio ambayo alistahili kuyapata.
Said PiePie,Nairobi.
No comments:
Post a Comment