Friday, 11 July 2014

UJERUMANI KUMENYANA NA URGENTINA KWENYE FAINALI


Baadhi ya wachezaji wa timu ya Ujerumani kwenye kambi ya mazoezi



      Ujerumani na Argentina zitakutana kwenye mechi ya fainali ya kombe la dunia Jumapili Julai tarehe 13 mjini Rio De Janeiro.Aidha mshindi ataweka kibindoni dola milioni 35 na wa pili $25 milioni, wa tatu $22milioni wa nne $20 milioni.Timu nne zilizoondolewa kwenye robo-fainali zitapokea $14 milioni kila mmoja, timu nane zilizong'olewa raundi ya pili $9 milioni na timu 16 zilizoondolewa raundi ya kwanza $8 milioni kila mmoja.     

Mchezaji wa safu ya mbele wa Argentina Angel Di Maria
Ujerumani ilifuzu kwa awamu ya  fainali baada ya kuwalaza Brazil mabao 7-1 na Argentina ikaiondoa Uholanzi mabao 4-2 kupitia mikwaju ya penalti ktika mechi ya nusu-fainali. Kwa jumla timu 32 zimeshiriki mashindano ya mwaka huu kwenye mechi 64 na wachezaji 736 wakajitosa uwanjani.Hii ni mara ya tatu Ujerumani na Argentina wanakutana fainali ya kombe la dunia, mara ya kwanza ikiwa mwaka wa 1986 nchini Mexico Argentina ikashinda 3-2 kisha wakapatana tena mwaka wa 1990 nchini Italia na Ujerumani ikalipiza kisasi kwa kuinyoa Argentina bao 1-0.

Argentina ilifuzu baada ya kushinda Uholanzi huku Ujerumani ikiwaadhibu Brazil 7-1.


Said PiePie,Nairobi.

No comments:

Post a Comment