Wednesday, 18 June 2014

MUAKA AELEKEA CITY STARS







Levy  Muaka ambaye amehamia City Stars
        Klabu ya Nairobi City Stars imemsajili kiungo wa kati Levy Muaka kutoka timu kutoka Vapor Fc kwa kandarsi ya miaka miwili.Taarifa hii imetolwa mapema hii leo na naibu kocha klabu ya City stars Joseph Jagero.
Aidha Jagero ameongeza kuwa wachezaji wengine ambao klabu yake imewapa kandarsi ni pamoja na  Oscar Mbugua na Wayne Ochieng
Nairobi city stars kwa sasa iko na alama 14 huku ikishikilia nafasi ya 14 katika jedwali la ligi ya primia humu nchini.


Said PiePie,Nairobi.

TUSKER YAMSAINI NG'ANG'A





   
Dennis Ng'ang'a aliyekua mchezaji wa Nairobi Stars hapo awali
          Tusker  FC  hatimaye wamnyakua  Dennis Ng'ang'a kutoka klabu Nairobi city kwa kandarasi ya  miaka 2.Kandarasi hii imetangazwa rasmi na mwelekezi  wa klabu ya wanamvinyo Charles Obiny akiongeza kuwa wamemtema raia wa Nigeria Governor aidha Jeffrey amelalama kuwa huduma za mchezaji huyo zimekua zikididimia kila uchao.

Said PiePie,Nairobi.


UBELGIJI YAINYAMAZISHA ALJERIA 2-1




    
Divock Origi katika pambano la jana didhi ya Aljeria

       Divock Origi ametia rekodi kuwa mkenya wa kwanza aliyebadilisha uraia kushiriki katika kombe la dunia. Origi alitimba dimbani dakika ya 58 nakujaza nafasi Romelu Lukaku
Marouane Fellaini na Dries Mertens waliisaidia Ubelgiji kunyakua ushindi dhidi ya Algeria katika mechi yao ya ufunguzi wa kombe la dunia huko Brazil.
Ubelgiji ilionekana kuwa moja ya timu ambazo zitashamiri huko Brazil hata hivyo iliwalazimu kusubiri hadi dakika ya 70, Ubeljiji kusawazisha bao la mapema la the Desert Foxes ambao walipata bao la penalti katika kipindi cha kwanza kupitia mchezaji Sofiane Feghouli.
Fellaini alifunga bao la kwanza; kwa kichwa katika dakika ya 70 huku Mertens akifunga la pili dakika kumi baadaye katika dakika ya 80 baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Eden Hazard.
Kevin De Bruyne alichangia vilivyo katika kupatikana kwa mabao yote ya Ubelgiji na bila shaka mkufunzi wa Ubeljiji, Marc Wilmotsatakuwa na kila sababu ya kufurahia alama hizo tatu kutoka kwa mechi ambayo ilionekana kuwa imemponyoka
Hazard na De Bruyne walikuwa na nafasi nyingi, ila safu ya ulinzi wa Algeria uliwazuia kumpitishia mshambulizi Romelu Lukaku mpira.
Madjid Bougherra na Rafik Halliche walilinda eneo la penalti la Algeria na kuyazuia mashambulizi ya wabeljiji .
Kufikia dakika ya 65, Wimots alikua amefanya mabadiliko mengine mawili; Divork Origi aliingia katika nafasi ya Lukaku naye Fellaini kwa upande wa Mousa Dembele.
Origi alipata nafasi nzuri pia, mapema baada ya kuingia kwake lakini kipa, M’Bolhi akausimamisha mkwaju wake wa chini.
Mchezaji chipukizi wa mwaka huu anatoka taifa la Cameroon Fabrice Olinga ambaye ana umri wa miaka 18 akifuatiwa na Luke Shaw kutokea Uingereza,hata hivyo rekodi ya mchezaji chipukiz ikuwahi kushiriki katika mechi za kombe la dunia ilivunjwa na Norman Whiteside aliyekuwa na umri wa miaka 18 aliposhiriki mecji za kombe la dunia mwaka wa 1982.

Said PiePie,Nairobi.

    

Tuesday, 17 June 2014

INGWE YAMTEMA MUSAJA

Hassan Mohamed ambaye ametemwa na Ingwe

     Strika  Hassan Mohammed almaarufu Musaja ametemwa na  AFC Leopards. Musaja hapo awali alichezea klabu ya  Kenya Revenue Authority (KRA) FC almetemwa kufuatia mchezo duni ambao alionyesha hapo awali
Habari hiz izimetolewa na Katibu wa mipango wa mipano Timothy Lilumbi wa klabu ya Ingwe.
Strika huyo alijiunga na Ingwe kwa kandarasi wa miak miwili kutoka KRA kwa kima cha shilingi alfu 200.


Said PiePie,Nairobi.

AGUERO ASEMA BADO YUPOYUPO MAN CITY




Sergio Aguero Strika wa Man City
    Mshambulizi matata wa timu ya Manchester City na  Argentina Sergio Aguero amepuzilia mbali madai kuwa anapani kuhamia klabu za Real Madrid na Barcelona.
Aguero aliyekua mchezaji wa  Atletico Madrid  hapo awali amezua uvumi mkubwa tangia ahamie Etihad 2011 kuwa ana miadi ya kurejea Uhispania.

Aguero alitoa tangazo rasmi katika  Radio Cadena Cope ya Uhispania pia alichapisha habari hizo katika jarida la The Citizens kuwa hana miadi yakugura Man City.
Aguero amefunga jumla ya mabao 28  mwaka 2013/2014 akiwa na Man City.


Said PiePie ,Nairobi