Wednesday, 18 June 2014

UBELGIJI YAINYAMAZISHA ALJERIA 2-1




    
Divock Origi katika pambano la jana didhi ya Aljeria

       Divock Origi ametia rekodi kuwa mkenya wa kwanza aliyebadilisha uraia kushiriki katika kombe la dunia. Origi alitimba dimbani dakika ya 58 nakujaza nafasi Romelu Lukaku
Marouane Fellaini na Dries Mertens waliisaidia Ubelgiji kunyakua ushindi dhidi ya Algeria katika mechi yao ya ufunguzi wa kombe la dunia huko Brazil.
Ubelgiji ilionekana kuwa moja ya timu ambazo zitashamiri huko Brazil hata hivyo iliwalazimu kusubiri hadi dakika ya 70, Ubeljiji kusawazisha bao la mapema la the Desert Foxes ambao walipata bao la penalti katika kipindi cha kwanza kupitia mchezaji Sofiane Feghouli.
Fellaini alifunga bao la kwanza; kwa kichwa katika dakika ya 70 huku Mertens akifunga la pili dakika kumi baadaye katika dakika ya 80 baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Eden Hazard.
Kevin De Bruyne alichangia vilivyo katika kupatikana kwa mabao yote ya Ubelgiji na bila shaka mkufunzi wa Ubeljiji, Marc Wilmotsatakuwa na kila sababu ya kufurahia alama hizo tatu kutoka kwa mechi ambayo ilionekana kuwa imemponyoka
Hazard na De Bruyne walikuwa na nafasi nyingi, ila safu ya ulinzi wa Algeria uliwazuia kumpitishia mshambulizi Romelu Lukaku mpira.
Madjid Bougherra na Rafik Halliche walilinda eneo la penalti la Algeria na kuyazuia mashambulizi ya wabeljiji .
Kufikia dakika ya 65, Wimots alikua amefanya mabadiliko mengine mawili; Divork Origi aliingia katika nafasi ya Lukaku naye Fellaini kwa upande wa Mousa Dembele.
Origi alipata nafasi nzuri pia, mapema baada ya kuingia kwake lakini kipa, M’Bolhi akausimamisha mkwaju wake wa chini.
Mchezaji chipukizi wa mwaka huu anatoka taifa la Cameroon Fabrice Olinga ambaye ana umri wa miaka 18 akifuatiwa na Luke Shaw kutokea Uingereza,hata hivyo rekodi ya mchezaji chipukiz ikuwahi kushiriki katika mechi za kombe la dunia ilivunjwa na Norman Whiteside aliyekuwa na umri wa miaka 18 aliposhiriki mecji za kombe la dunia mwaka wa 1982.

Said PiePie,Nairobi.

    

No comments:

Post a Comment