Tuesday, 17 June 2014

AGUERO ASEMA BADO YUPOYUPO MAN CITY




Sergio Aguero Strika wa Man City
    Mshambulizi matata wa timu ya Manchester City na  Argentina Sergio Aguero amepuzilia mbali madai kuwa anapani kuhamia klabu za Real Madrid na Barcelona.
Aguero aliyekua mchezaji wa  Atletico Madrid  hapo awali amezua uvumi mkubwa tangia ahamie Etihad 2011 kuwa ana miadi ya kurejea Uhispania.

Aguero alitoa tangazo rasmi katika  Radio Cadena Cope ya Uhispania pia alichapisha habari hizo katika jarida la The Citizens kuwa hana miadi yakugura Man City.
Aguero amefunga jumla ya mabao 28  mwaka 2013/2014 akiwa na Man City.


Said PiePie ,Nairobi

No comments:

Post a Comment