Monday, 16 June 2014

GOR YAMSAINI OTIENO




       
 
Timothy Otieno Talanta Fc

     Klabu ya Gor mahia ametia mkataba wa miezi sita na kiungo wa kati  wa Talanta FC Timothy Otieno,Kiungo huyo anauwezo mkubwa na aliisaidia klabu yake hapo awali kunyakua mataji kadhaa hatua iliyopelekea klabu nyingi kummezea mate. Kiungo huyo.Alifuzu kutoka National Youth Talent Academy (NYTA) pia ni mwanafunzi wa zamani wa shule ya upili ya Kakamega.

Said PiePie,Nairobi.

GOAL TECHNOLOGY KUTUMIKA EPL MSIMU UJAO








         Klabu za ligi kuu ya soka nchini England zimeafikiana kutumia teknolojia ya camera katika maamuzi ya mchezo wa soka kuanzia msimu ujao.
Kampuni ya Uingereza ya Hawk-Eye imepewa mkataba wa kufunga vifaa maalumu kwenye viwanja vyote 20 vya timu za ligi kuu nchini England.
Hawk-Eye inajulikana kwa  teknolojia kama hiyo kwenye mchezo wa Tenesi na Kriketi,ambapo camera maalumu huweza kutambua iwapo mpira umegusa mstari ama la na kumjulisha mwamuzi na wasaidizi wake ndani ya sekunde chache.
Chama cha soka nchini England FA,kitafunga vifaa hivyo kwenye uwanja wa Wembley tayari kwa kutumika kwenye mchezo wa ngao ya jamii hapo mwezi wa nane mwaka huu.
Viwanja vya timu 17 zitakazosalia ligi kuu na zile 3 zitakazopanda daraja vitawekewa teknolojia hiyo na shughuli nzima itachukua wiki sita kukamilika.Msukumo wa kutumia teknolojia maalumu ya kutambua goli ilipata nguvu baada England kukataliwa goli lao la kusawazisha walipocheza na Ukraine,Mchezo ambao England walifungwa bao moja kwa bila kwenye michuano ya kombe la mataifa barani Ulaya mwaka 2012, Ambapo mwezi mmoja baadaye bodi ya vyama vya soka vya kimataifa (IFAB) katika kikao chake mjini Zurich kilipitisha teknolojia mbili ili zitumike kwenye michezo ya soka.Rais wa FIFA Sepp Blater amesema kukataliwa kwa goli la Frank Lampard kwenye mechi ya robo fainali kati ya England na Ujerumani mwaka 2010 katika michuano ya kombe la dunia,kulichangia kwa kiasi kikubwa maamuzi ya shirikisho hilo kupitisha sheria ya matumizi ya teknolojia ya kutambua goli.
Chama cha soka cha England kimesema teknolojia hiyo itaaanza kutumika msimu ujao.Kwa sasa Goal  Technology inatumika katika michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.

Said PiePie,Nairobi.

TUSKER YAZIDI KUNOGA



Tusker  Fc washerehekea ushindi wao dhidi ya Ingwe
     Nahodha wa  Tusker Fc  almaarufu wanamvinyo Samwel Odhiambo amesema kuwa timu yake iko katika hali nzuri yaku kung’ang’ania taji la KPL msimu huu alisema haya mapema hii leo.Hapo jana Wanamvinyo hao ilicharaza Inmgwe mabao 2-1 katika mechi za Nane bora katika  uchanjaa wa Kinoru,Meru.Kwa sasa Tusker inashikilia nafasi ya tatu na alama 27 katika jedwali la ligi ya primia humu nchini.



Said PiePie,Nairobi.

Friday, 13 June 2014

MIENO AHAMIA INGWE


 


 
Humphrey Mieno  aliyekua mchezaji wa Sofapaka

         Ni rasmi kuwa Humphrey Mieno amejiunga na kikosi cha AFC Leopards baada ya kugura timu ya  Sofapaka almaarufu Batoto Ba Mungu kwa kandarasi ya miaka miwili.Wanamvinyo Tusker Fc pia walikua wakimmezea mate lakini Ingwe wakaonyesha ukali wamakucha baada ya kumnyakua haraka.Rais wa Sofapaka Elly Kalekwa amesema kuwa  uhamisho huo ulifanywa hapo jana.Uhamisho huo uliendeshwa na shirika la International Sports and Entertainment Management Limited (ISEML).

Said PiePie,Nairobi.

UHURU AFADHILI STARS KUELEKEA BRAZIL



Rais Kenyatta akiwa na kikosi cha Harambee Stars
         Rais  Uhuru Kenyatta amekifadhili kikosi cha Harambe Stars kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la duniaHafla hiyo,ilifanyika katika ikulu ya Rais ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa vyeti vya usafiri kwenda Brazil.
Kenyatta na mkewe  Margaret Kenyatta wamekifadhili kikosi hicho dola elfu 40. Aidha Rais amesema lengo lake hasa ni kuwapa matumaini na motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka nchini Kenya.Rais  hakwenda na kikosi hicho bali aliwahauri wachezaji hao kuwa mabalozi wema wa Kenya nchini Brazil.Ufadhili huo unawadia miezi sita baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara wa kocha wa timu hiyo kwa miakja miotano ijayo.
Kenya haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia lakini ziara hii kwa vijana wa Harambee Stars itawafungua macho huku wakiwa na azma ya kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili na kujiandaa kuchuana na Lesotho tarehe 18 mwezi ujao.Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji ; Clifton Miheso, David Owino, Joackins Atudo, Abud Omar, James Situma, Wilson Obungu, Allan Wanga, Jacob Keli, Edwin Lavatsa, Francis Kahata, Joe Muiruri Gachoka, Jerim Onyango, Musa Mohammed, Hillary Kimaru Kipchillat, Samuel Njenga Miringu, Duncan Ochieng’, Dennis Oliech, Paul Mungai,
Wakiwemo maafisa wa usimamizi na kocha  Adel Amrouche, James Nandwa, Jacob Ghost Mulee, Kennedy Odhiambo, Elly Mukolwe, Daniel Francis Irukan, Julius Maina Kigaga.

Said PiePie,Nairobi

MWANAMICHEZO: BRAZIL WAILAZA KROATIA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI

MWANAMICHEZO: BRAZIL WAILAZA KROATIA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI: Uga wa Corithians Sao Paulo unachukua mashabiki 61,500     

Sherehe za Ufunguzi wa Kombe la Dunia Brazil 2014 ziliaanza  ...

BRAZIL WAILAZA KROATIA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI


   
 
Uga wa Corithians Sao Paulo unachukua mashabiki 61,500
     Sherehe za Ufunguzi wa Kombe la Dunia Brazil 2014 ziliaanza  kwa mbwembwe ya aina yake huku  mwimbaji wa kimataifa Jinnifer Lopez akipamba jukwaa Katika uga  wa Corithians Sao Paolo.Timu ya taifa la Croatia iliwachezesha : Pletikosa; Srna, Ćorluka, Lovren, Vrsaljko; Modrić, Rakitić, PeriÅ¡ić, Brozović; Olić, Jelavić huku nao wapinzani wao Brazil wakiwashirikisha katika kikosi chao : Cesar; D.Alves, T.Silva, D.Luiz, Marcelo; Paulinho, L.Gustavo; Hulk, Oscar, Neymar; Fred. 





Marcelo Vieira  anayeichezea Real Madrid
Mercelo alijifunga katika kipindi cah kwanza na kuipa Croatia bao la kwanza .
Neymar aliifungia bao la kwanza na  pili Brazil kupitia kwa mkwaju wa penalti hata hivo maswali yanazidi kuibuka  kuhusiana na penalti hiyo.Mchezaji huyo  aliiandikisha rekodi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya Njano kwa kumpiga kumbo Modric katika mechi za kombe la dunia mwaka huu.Katika dakika ya 47 Neymar alifanyiwa badiliko huku mchezaji Ramires anayeisakatia Chelsea akijaza pengo lake.Oscar amhakikishia kocha Luiz Felipe Scolari ushindi muhimu katika mechi ya ufunguzi wa dhidi ya Croatia kwa kupachika kimiani bao la tatu na la ushindi.
Kocha wa Croatia Niko Kovac ambaye alikuwa na hasira amesema mwamuzi kutoka Japan Yuichi Nishimura aliyesimamia pambano hilo la jana alikuwa hayuko katika kiwango chake, baada ya kutoa penalti kwa Brazil ambayo imebishaniwa na kubadilisha kabisa mwelekeo wa mchezo huo wa ufunguzi.
Croatia wako katika nafasi ya 18 ya orodha ya FIFA ya timu bora duniani , ilikuwa ikijaribu kuzuwia na kuwatuliza Brazil katika kipindi cha pili hadi pale refa Yuichi Nishimura alipoamua upigwe mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wa Brazil Fred kuanguka wakati akipambana na mlinzi wa Croatia Dejean Lovren
Hii  leo Simba wa Nyika , Cameroon , wataingia uwanjani kupambana na Mexico katika mchezo mwingine wa kundi A, wakati mabingwa watetezi Uhispania inaanza kampeni ya kurelijesha taji hilo mjini Madrid kwa kupambana na Uholanzi katika mchezo wa kundi B.

Said PiePie,Nairobi.



Thursday, 12 June 2014

WACHEZAJI KADHAA KUKOSA MECHI ZA LIGI YA PREMIA






    Wachezaji watatu wa ligi ya primia watatakosa mechi katika  juma la 15 baada ya kuonyeshwa kadi za njano.Timu ya SoNy Sugar itakosa hudumu za Edwin Oduor  baada ya kupata kadi 5 za manjano wakati  wa mechi kati yao na Muhoroni katika Uga wa Awendo mnamo Juni 15,huku wanamanasi Thika United watakosa huduma za mlindalango Dennis Odhiambo wakati wa mchuano wao na Mathare United katika uga wa Nyayo siku ya City Stadium.Odhiambo anakadi 5 za manjano.

Said PiePie,Nairobi