Friday, 13 June 2014

BRAZIL WAILAZA KROATIA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI


   
 
Uga wa Corithians Sao Paulo unachukua mashabiki 61,500
     Sherehe za Ufunguzi wa Kombe la Dunia Brazil 2014 ziliaanza  kwa mbwembwe ya aina yake huku  mwimbaji wa kimataifa Jinnifer Lopez akipamba jukwaa Katika uga  wa Corithians Sao Paolo.Timu ya taifa la Croatia iliwachezesha : Pletikosa; Srna, Ćorluka, Lovren, Vrsaljko; Modrić, Rakitić, Perišić, Brozović; Olić, Jelavić huku nao wapinzani wao Brazil wakiwashirikisha katika kikosi chao : Cesar; D.Alves, T.Silva, D.Luiz, Marcelo; Paulinho, L.Gustavo; Hulk, Oscar, Neymar; Fred. 





Marcelo Vieira  anayeichezea Real Madrid
Mercelo alijifunga katika kipindi cah kwanza na kuipa Croatia bao la kwanza .
Neymar aliifungia bao la kwanza na  pili Brazil kupitia kwa mkwaju wa penalti hata hivo maswali yanazidi kuibuka  kuhusiana na penalti hiyo.Mchezaji huyo  aliiandikisha rekodi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya Njano kwa kumpiga kumbo Modric katika mechi za kombe la dunia mwaka huu.Katika dakika ya 47 Neymar alifanyiwa badiliko huku mchezaji Ramires anayeisakatia Chelsea akijaza pengo lake.Oscar amhakikishia kocha Luiz Felipe Scolari ushindi muhimu katika mechi ya ufunguzi wa dhidi ya Croatia kwa kupachika kimiani bao la tatu na la ushindi.
Kocha wa Croatia Niko Kovac ambaye alikuwa na hasira amesema mwamuzi kutoka Japan Yuichi Nishimura aliyesimamia pambano hilo la jana alikuwa hayuko katika kiwango chake, baada ya kutoa penalti kwa Brazil ambayo imebishaniwa na kubadilisha kabisa mwelekeo wa mchezo huo wa ufunguzi.
Croatia wako katika nafasi ya 18 ya orodha ya FIFA ya timu bora duniani , ilikuwa ikijaribu kuzuwia na kuwatuliza Brazil katika kipindi cha pili hadi pale refa Yuichi Nishimura alipoamua upigwe mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wa Brazil Fred kuanguka wakati akipambana na mlinzi wa Croatia Dejean Lovren
Hii  leo Simba wa Nyika , Cameroon , wataingia uwanjani kupambana na Mexico katika mchezo mwingine wa kundi A, wakati mabingwa watetezi Uhispania inaanza kampeni ya kurelijesha taji hilo mjini Madrid kwa kupambana na Uholanzi katika mchezo wa kundi B.

Said PiePie,Nairobi.



No comments:

Post a Comment