![]() |
Humphrey Mieno aliyekua mchezaji wa Sofapaka |
Ni rasmi kuwa Humphrey Mieno amejiunga na kikosi cha AFC Leopards baada ya kugura timu ya Sofapaka almaarufu Batoto Ba Mungu kwa kandarasi ya miaka miwili.Wanamvinyo Tusker Fc pia walikua wakimmezea mate lakini Ingwe wakaonyesha ukali wamakucha baada ya kumnyakua haraka.Rais wa Sofapaka Elly Kalekwa amesema kuwa uhamisho huo ulifanywa hapo jana.Uhamisho huo uliendeshwa na shirika la International Sports and Entertainment Management Limited (ISEML).
Said PiePie,Nairobi.
No comments:
Post a Comment