![]() |
Rais Kenyatta akiwa na kikosi cha Harambee Stars |
Rais Uhuru Kenyatta
amekifadhili kikosi cha Harambe Stars
kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la duniaHafla hiyo,ilifanyika katika ikulu ya Rais ambapo wachezaji kumi na
moja wa timu hiyo walikabidhiwa vyeti vya usafiri kwenda Brazil.
Kenya haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia lakini ziara hii kwa vijana wa Harambee Stars itawafungua macho huku wakiwa na azma ya kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili na kujiandaa kuchuana na Lesotho tarehe 18 mwezi ujao.Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji ; Clifton Miheso, David Owino, Joackins Atudo, Abud Omar, James Situma, Wilson Obungu, Allan Wanga, Jacob Keli, Edwin Lavatsa, Francis Kahata, Joe Muiruri Gachoka, Jerim Onyango, Musa Mohammed, Hillary Kimaru Kipchillat, Samuel Njenga Miringu, Duncan Ochieng’, Dennis Oliech, Paul Mungai,
Wakiwemo maafisa wa usimamizi na kocha Adel Amrouche, James Nandwa, Jacob Ghost Mulee, Kennedy Odhiambo, Elly Mukolwe, Daniel Francis Irukan, Julius Maina Kigaga.
Said PiePie,Nairobi
No comments:
Post a Comment