Friday, 13 June 2014

MIENO AHAMIA INGWE


 


 
Humphrey Mieno  aliyekua mchezaji wa Sofapaka

         Ni rasmi kuwa Humphrey Mieno amejiunga na kikosi cha AFC Leopards baada ya kugura timu ya  Sofapaka almaarufu Batoto Ba Mungu kwa kandarasi ya miaka miwili.Wanamvinyo Tusker Fc pia walikua wakimmezea mate lakini Ingwe wakaonyesha ukali wamakucha baada ya kumnyakua haraka.Rais wa Sofapaka Elly Kalekwa amesema kuwa  uhamisho huo ulifanywa hapo jana.Uhamisho huo uliendeshwa na shirika la International Sports and Entertainment Management Limited (ISEML).

Said PiePie,Nairobi.

UHURU AFADHILI STARS KUELEKEA BRAZIL



Rais Kenyatta akiwa na kikosi cha Harambee Stars
         Rais  Uhuru Kenyatta amekifadhili kikosi cha Harambe Stars kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la duniaHafla hiyo,ilifanyika katika ikulu ya Rais ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa vyeti vya usafiri kwenda Brazil.
Kenyatta na mkewe  Margaret Kenyatta wamekifadhili kikosi hicho dola elfu 40. Aidha Rais amesema lengo lake hasa ni kuwapa matumaini na motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka nchini Kenya.Rais  hakwenda na kikosi hicho bali aliwahauri wachezaji hao kuwa mabalozi wema wa Kenya nchini Brazil.Ufadhili huo unawadia miezi sita baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara wa kocha wa timu hiyo kwa miakja miotano ijayo.
Kenya haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia lakini ziara hii kwa vijana wa Harambee Stars itawafungua macho huku wakiwa na azma ya kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili na kujiandaa kuchuana na Lesotho tarehe 18 mwezi ujao.Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji ; Clifton Miheso, David Owino, Joackins Atudo, Abud Omar, James Situma, Wilson Obungu, Allan Wanga, Jacob Keli, Edwin Lavatsa, Francis Kahata, Joe Muiruri Gachoka, Jerim Onyango, Musa Mohammed, Hillary Kimaru Kipchillat, Samuel Njenga Miringu, Duncan Ochieng’, Dennis Oliech, Paul Mungai,
Wakiwemo maafisa wa usimamizi na kocha  Adel Amrouche, James Nandwa, Jacob Ghost Mulee, Kennedy Odhiambo, Elly Mukolwe, Daniel Francis Irukan, Julius Maina Kigaga.

Said PiePie,Nairobi

MWANAMICHEZO: BRAZIL WAILAZA KROATIA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI

MWANAMICHEZO: BRAZIL WAILAZA KROATIA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI: Uga wa Corithians Sao Paulo unachukua mashabiki 61,500     

Sherehe za Ufunguzi wa Kombe la Dunia Brazil 2014 ziliaanza  ...

BRAZIL WAILAZA KROATIA KATIKA MECHI YA UFUNGUZI


   
 
Uga wa Corithians Sao Paulo unachukua mashabiki 61,500
     Sherehe za Ufunguzi wa Kombe la Dunia Brazil 2014 ziliaanza  kwa mbwembwe ya aina yake huku  mwimbaji wa kimataifa Jinnifer Lopez akipamba jukwaa Katika uga  wa Corithians Sao Paolo.Timu ya taifa la Croatia iliwachezesha : Pletikosa; Srna, Ćorluka, Lovren, Vrsaljko; Modrić, Rakitić, PeriÅ¡ić, Brozović; Olić, Jelavić huku nao wapinzani wao Brazil wakiwashirikisha katika kikosi chao : Cesar; D.Alves, T.Silva, D.Luiz, Marcelo; Paulinho, L.Gustavo; Hulk, Oscar, Neymar; Fred. 





Marcelo Vieira  anayeichezea Real Madrid
Mercelo alijifunga katika kipindi cah kwanza na kuipa Croatia bao la kwanza .
Neymar aliifungia bao la kwanza na  pili Brazil kupitia kwa mkwaju wa penalti hata hivo maswali yanazidi kuibuka  kuhusiana na penalti hiyo.Mchezaji huyo  aliiandikisha rekodi kwa kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya Njano kwa kumpiga kumbo Modric katika mechi za kombe la dunia mwaka huu.Katika dakika ya 47 Neymar alifanyiwa badiliko huku mchezaji Ramires anayeisakatia Chelsea akijaza pengo lake.Oscar amhakikishia kocha Luiz Felipe Scolari ushindi muhimu katika mechi ya ufunguzi wa dhidi ya Croatia kwa kupachika kimiani bao la tatu na la ushindi.
Kocha wa Croatia Niko Kovac ambaye alikuwa na hasira amesema mwamuzi kutoka Japan Yuichi Nishimura aliyesimamia pambano hilo la jana alikuwa hayuko katika kiwango chake, baada ya kutoa penalti kwa Brazil ambayo imebishaniwa na kubadilisha kabisa mwelekeo wa mchezo huo wa ufunguzi.
Croatia wako katika nafasi ya 18 ya orodha ya FIFA ya timu bora duniani , ilikuwa ikijaribu kuzuwia na kuwatuliza Brazil katika kipindi cha pili hadi pale refa Yuichi Nishimura alipoamua upigwe mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wa Brazil Fred kuanguka wakati akipambana na mlinzi wa Croatia Dejean Lovren
Hii  leo Simba wa Nyika , Cameroon , wataingia uwanjani kupambana na Mexico katika mchezo mwingine wa kundi A, wakati mabingwa watetezi Uhispania inaanza kampeni ya kurelijesha taji hilo mjini Madrid kwa kupambana na Uholanzi katika mchezo wa kundi B.

Said PiePie,Nairobi.



Thursday, 12 June 2014

WACHEZAJI KADHAA KUKOSA MECHI ZA LIGI YA PREMIA






    Wachezaji watatu wa ligi ya primia watatakosa mechi katika  juma la 15 baada ya kuonyeshwa kadi za njano.Timu ya SoNy Sugar itakosa hudumu za Edwin Oduor  baada ya kupata kadi 5 za manjano wakati  wa mechi kati yao na Muhoroni katika Uga wa Awendo mnamo Juni 15,huku wanamanasi Thika United watakosa huduma za mlindalango Dennis Odhiambo wakati wa mchuano wao na Mathare United katika uga wa Nyayo siku ya City Stadium.Odhiambo anakadi 5 za manjano.

Said PiePie,Nairobi

INGWE YAFUZU FAINALI ZA NANE BORA






 

      Timu ya AFC Leopards hapo jana ilinyakua ushindi baada ya kuwalaza kcb 3-0 katika mchuano wa timu nane bora katika mechi ya nusu fainali.Austin Ikenna ,Jacob Keli  and Bernard Mang’oli  waliisaidia Leopards kunyakua ushindi huo. Wanabenki KCB walionyesha mchezo mzuri katika kipindi cha kwanza hata hivyo walikumbwa na utasa wa mabao.KCB walifanya badiliko katika dakika za kwanza za 12 baada ya kiungo wao wa kati Hedson Mauda kujeruhiwa pengo  lake lilijazwa na Ronald Musana aliyesajiliwa majuzi
          Mabeki ya KCB walizembea mnamo dakika ya 40 nakumpa  fursa Paul Were aliipenyeza pasi ya kimanjaro kwake Bernard Mangoli wingi wa kushoto naye hakusita ila alimpeleka madukani mlinda lango wa KCB Caleb Wafula huku akiiandikia Ingwe bao la pili
Kipindi cha pili kilianza na mabadiliko huku Joseph Shikokoti akitolewa nje na nafasi yake ikimilikiwa na  Eric Masika.Kwa sasa ingwe imejikatia tiketi ya fainali itakapo kutana na wanamvinyo Tusker FC Juni 15.

Said PiePie, Nairobi

KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014






    Rais wa Brazil Dilma Rousseff amewaomba  wananchi nchini humo kuungana pamoja kwa ajili ya Kombe la Dunia la 2014, akisema taifa liko tayari licha ya Migomo na maandamano ambayo yameshuhudiwa nchini humo.Katika hotuba yake iliyorushwa kwenye televisheni kabla ya ufunguzi wa tamasha hilo, rais huyo amesema macho ya ulimwengu mzima yanaiangazia Brazil akisema nchi hiyo ilikabiliana na changamoto kubwa na sasa iko tayari ndani na nje ya viwanja kwa ajili ya burudani hilo la soka.
Huku hayo yakijiri vitisho vilivyokuwepo vya  mgomo vimeondolewa kwa muda huku wafanyakazi wa treni za chini ya ardhi mjini Rio wakiufutilia mbali mgomo wao baada ya kupewa nyongeza ya mshahara ya asilimia 8. Mgomo wa siku tano wa usafiri mjini Sao Paulo pia ulisitishwa Jumatatu wiki hii, ijapokuwa huenda ukarejea tena wakati michuano itakapoanza kama wafanyakazi waliopigwa kalamu hawatorudishwa kazini.
     Sherehe za ufunguzi wa dimba hilo zinaandaliwa katika uwanja wa Corinthians Arena, mjini Sao Paulo hii leo, miongoni mwa wageni watakaohudhuria ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon pamoja na viongozi 12 wa nchi na serikali.
Baada ya sherehe za ufunguzi, vijana wa kocha Luiz Felipe Scolari, watashuka dimbani kupambana na Croatia katika mechi ya ufunguzi ya Kundi A. Na kama wenyeji hao wataweza kufika katika fainali na kunyakua taji hilo mnamo Julai 13, watakuwa timu ya tatu pekee iliyocheza mechi ya ufunguzi kuwahi kufanya hivyo.
Katika michuano 19 ya Kombe la Dunia,  Italia pekee  mwaka wa 1934 na England mwaka wa 1966 zilizowahi kucheza mechi ya kwanza na  kushinda katika fainali. Zaidi ya wanajeshi na polisi 150,000 watashika doria k wakati wa dimba hilo.

Said PiePie,Nairobi