 |
Ujerumani watawazwa mabingwa wa kombe duina 2014 nchini Brazil |
Shangwe,nderemo,vifijo ziligubika anga ya uga wa Estadio Mineirao mjini Rio de Janeiro Brazil jana baada ya Vijana wa Joachim LoewUjerumani kuwalaza 1-0 Argentina na kutawazwa mabingwa wa kombe la dunia 2014.Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani
Joachim Loew amesema ndoto ya timu kutwaa kombe la dunia ilitimia hapo jana usiku. Mchezaji kiungo Mario Goetze-Super
Mario aliingia kwenye madaftari ya vya
historia pale alipopachika goli la ushindi katika fainali za kombe la dunia,
lililoipatia Ujerumani ubingwa wa dunia. Nyota huyo wa klabu ya Bayern Munich
alitegua kitendawili cha ubingwa katika dakika za nyoneza (113) na kuinyamanzisha Argentina, huku ndoto ya
Lionel Messi ya kufuata nyayo za nguli Diego Maradona ikiishia kwa kushindwa.
Ujerumani sasa imeshinda kombe la
dunia mara nne, na kulifanya taifa hilo kubwa duniani kuwa nyuma tu ya Brazil
yenye rekodi ya ushindi mara tano. Muda wa maamuzi wa fainali hiyo iliyojawa na
msisimko na magoli yaliyofungwa kwa ustadi mkubwa ulikuja wakati timu hizo
zikinyemelewa na mikwaju ya penati mbele ya watazamaji 74,738 katika uwanja
maarufu wa Maracana mjini Rio de Janeiro.Mchezaji bora wa mechi hiyo ya
fainali Goetze aliituliza kifuani krosi ya Andre Schuerrle na bila kufanya
ajizi akasukuma mkwaju uliyomduwaza mlinda mlango wa Argentina Sergio Romero,
kwa goli la ushindi lililomfanya nahodha Philip Lahm kubeba kombe la dunia.
 |
Mario Gotze aadhimisha bao lak |
Ujerumani ambayo iliinyeshea Brazil
mvua ya magoli 7 -1 katika mchezo wa nusu fainali, imekuwa timu ya kwanza ya
Ulaya kubeba kombe la dunia katika Amerika ya Kusini. Walianza kushinda taji
hilo mwaka 1954, na kulirudia mwaka 1974 na 1990. Wamekuwa wakilikosakosa ama
kwa kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali au fainali katika miaka ya hivi
karibuni.Lionel Messi hakucheza kama
alivyotarajiwa. Kiungo wa kati Javier Mascherano alisema ni vigumu kueleza,
kwani walifanya kila kitu kushinda na walikuwa na nafasi nzuri zaidi.Aidha Messi, Gonzalo Higuain na
Rodrigo Palacio walikosa nafasi nzuri cha juu wakati kichwa cha Benedikt
Hoewedes kiligonga mwamba kwa upande wa Ujerumani mbele ya maelfu ya mashabiki
wakiwemo rais wa Ujerumani Joachim Gauck, Kansela Angela Merkel, rais wa Urusi
Vladmir Putin na mwenyeji wao rais wa Brazil Dilma Roussef.
 |
Mbwembwe za mashabiki wa Ujerumani |
Wakiwa wamebeba kombe mikononi mwao,
wachezaji wa Ujerumani waliimba pamoja na mashabiki wao, wimbo maarufu wa Am
Tag Wie Diesen (Katika siku kama hii) uliyopigwa na bendi ya Ujerumani ya Die
Toten Hosen na kuchezwa uwanjani. Ilikuwa ndoto iliyotimia baada ya subira ya
miaka mingi.Kufuatia ushindi huo Ujerumani
walinyakua taji la nne la dunia.Kipa wa Ujerumani Manuel Nuer alitawazwa kuwa
kipa bora na akatuzwa ''Golden Glove''.Rais wa Urusi Vlamir Putin alipokea
ithibati rasmi ya kuandaa makala yajayo ya kombe la dunia kutoka kwa rais wa
FIFA.Rais wa Urusi Vladimir Putin
alikuwepo Maracana kwa mualiko wa rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa Brazil
Dilma Rousseff. Makala yajayo ya kombe la dunia yataandaliwa nchini Urusi mwaka
wa 2018.
Said PiePie,Nairobi.