Friday, 4 July 2014

KASHFA YA VYETI GHUSHI NIGERIA


  
   
Mwenyekiti wa Shirikisho la soka nchini Nigeria,Aminu Maigari
       I
dara ya ujasusi nchini Nigeria imemtia nguvuni mwenyekiti wa shirikisho nchini humo   
Aminu Maigari  kwa madai ya vyeti ghushi.Inaripotiwa kuwa Maigari imetiwa nguvuni baada ya kuwasaili katika uwanja wa michezo wa Nnamdi Azikiwe mjini Abuja,Keshi hiyo hapo awali ilikua ikiendeshwa katika Mahakam ya Jos siku ya jumatatu.Aidha duru zinaripoti kuwa Maigari amekua akiendesha shughuli za ofisi na vyeti ghushi habari hizi pia zimetolewa na mtandao wa  www.gongnews.net

 Said PiePie,Nairobi.

BRAZIL KUMENYANA NA COLOMBIA



Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil alamaarufu Samba Boys
   B
razil na Colombia zitamenyana kwenye mchezo wa robo fainali ya  Kombe la Dunia hii leo mchuano huo utakaragaziwa  Uwanjani Castelao mjini Fortaleza.Mara ya mwisho Colombia kuilaza  Brazil ilikuwa mwaka 1991. Lakini, kipute hicho cha robo fainali ya Kombe la Dunia kinaikuta Colombia ikiwa kwenye ubora mkubwa na kuundwa na nyota makini akiwemo Rodriguez, Juan Cuadrado na Jackson Martinez na kuwafanya Brazil kuwa kwenye presha kubwa sana.Cuadrado, ndiye mchezaji aliyepiga pasi nyingi zilizozaa mabao kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia, akiwa amechangia mabao manne kwa kikosi cha Colombia.Kwenye hatua ya 16 bora, Brazil ilipata shida dhidi ya Chile na kufanikiwa kuwatupa nje kwa mikwaju ya penalti 3-2, wakati Colombia iliichapa Uruguay kiulaini mabao 2-0, shukrani kwa mabao hatari ya Rodriguez na kazi nzuri ya staa wa taifa hilo, Cuadrado.Utamu wa mchezo huo utazikutanisha timu mbili zinazobebwa na mastaa vijana, Neymar kwa upande wa Brazil na Rodriguez kwa Colombia. Kwenye fainali hizo, Neymar ametikisa nyavu mara mbili, moja pungufu ya mpinzani wake wa leo, James Rodriguez. 


Radamel Falcao Strika wa Colombia
Robo fainali hiyo itatanguliwa na ile kati ya Ufaransa na Ujerumani itakayopigwa kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro. Mechi hiyo ya Ufaransa na Ujerumani ni ya kihistoria.
Timu hizo mbili ziliwahi kumenyana kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 1982, ambapo Wajerumani walishinda kwa mikwaju ya penalti. Ufaransa itaingia kwenye mchezo huo ikitaka kulipa kisasi, lakini jambo hilo litafanywa na wachezaji 21 kati ya 23 kwenye kikosi hicho cha Les Bleus ambao walikuwa hawajazaliwa wakati timu yao ikifungwa kwa penalti na Ujerumani katika fainali hizo.Kiungo Blaise Matuidi atabeba majukumu ya Ufaransa kwenye sehemu ya kiungo sambamba na Paul Pogba na Yohan Cabaye, ambao watakuwa kwenye vita ya nguvu dhidi ya Toni Kroos, ambaye amefunika kwa kupiga pasi katika fainali hizo za Brazil.Aidha mechi nyingine za hatua ya robo fainali zitaendelea kesho,ambapo Argentina itakajimwaya uwanjani  na Ubelgiji na Uholanzi itakapokwaruzana na Costa Rica.


Said PiePie,Nairobi


"STARS HAISAFIRI KWA MATATU" ASEMA NYAMWEYA



Sam Nyamweya Mwenyekiti wa FKF

      Mwenyekiti wa shirikisho la kandanda nchini Sam Nyamweya anamtaka Gavana  wa Machakos Alfred Mutua aombe msamaha kwa matamshi aliyoyatoa kuwa timu ya taifa ya  Harambee Stars hutumia magari aina ya Matatu kwa usafiri wake hii ni kulingana na ripoti iliyochapishwa kwa mtandao wa shirikisho la FKF.Wakati uo huo Nyamweya alipinga madai hayo akisema kuwa Harambee Stars hutumia usafiri waa ndege.Huku hayo yakijiri Stars wanapania kumenyana na timu ya taifa ya Lesotho katika mchuano wa kufuzu katika mechi za AFCON 2015 Julai 19 Maseru Lesotho huku mchuano wa nyumbani ukiratibiwa kucharazwa Agosti 3 mjini Nakuru.


Said PiePie,Nairobi

MAFUA YAVAMIA UTIMU YA UJERUMANI


Baadhi ya wachezaji wa Kikosi cha Ujerumani
      U
jerumani, imesema kuwa wachezaji saba wawanaugua mafua hili linajiri saa chache tu kabla ya mchuano kati yao na Ufaransa.Kocha wa Ujerumani Joachim Low anasema kuwa wengi wanaumwa na koo ingawa hakutaja majina ya wachezaji hao.Mats Hummels na Christoph Kramer waliugua mapema wiki hii huku Mat akikosa mechi ya muondoano dhidi ya Algeria Jumatatu.Low anaamini kuwa mazingira ya Brazil na safari za hapa na pale nchini humo pamoja na mvua kubwa ndio sababu ya wachezaji wake kuugua .Aidha kocha huyo amesema kikosi chake kikiongangari kwa mechi ya leo fauka ya tishio la mafua


Said PiePie,Nairobi.



Thursday, 3 July 2014

ORIGI KUELEKEA UINGEREZA MSIMU UJAO



Divorc Origi,anayesakatia kabumbu Ubelgiji na Lille ya Ufaransa
      Mjombake Divorc Origi, Austin Oduor, amesema strika  huyo wa  taifa ya Ubelgiji anapania kuelekea Uingerza msimu ujao.Aidha Oduor, ameongeza kuwa strika yuko katika hali nzuri ya kuelekea Uingereza msimu ujao.Origi, mwenye umri wa miaka 19 ameonyesha mchezo mzuri kwenye mashindano ya kandanda ya kombe la dunia nchini Brazil, na kwa mara ya kwanza alicheza dakika zote tisini dhidi ya Marekani kwenye mechi yao ya raundi ya pili, na hatimaye Romelu Lukaku akaingia uwanjani naye Origi akapumzika.Miongoni mwa timu za ligi kuu ambazo zinammezea  Origi mate ni Liverpool, Tottenham Hotspurs na Arsenal lakini kuna dalili Liverpool itamnasa kinda huyo ambaye alizaliwa Ubelgiji wakati babake Mike Okoth, raia wa Kenya, alipokuwa akicheza kandanda ya kulipwa nchini humo.Origi mwenyewe anasema ana hamu sana ya kushiriki ligi kuu ya England bora apate klabu kitakachomfurahisha.Babake Origi ni shabiki sugu wa Liverpool hivyo basi huenda akamshawishi mwanawe ajiunge na bingwa hao mara 18 wa ligi kuu ya England.Lakini kabla mashindano ya kombe la dunia yaanze Okoth alisema atampa Origi uhuru wa kuamua ni klabu kipi anataka kuchezea England endapo atagura Lille ya Ufaransa.

Said PiePie,Nairobi        

Tuesday, 1 July 2014

"RAMADHAN HAIKUTUADHIRI" ALGERIA WAKIRI.


 
Mlindalango wa Algeria Rais M’Bolh
      Rais M’Bolhi golkipa wa Algeria amekanusha madai wachezahi wao walishindwa na Ujerumani kutokana na wao kuwa wadhaifu kwa kufunga saumu.M’Bolhi ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo ambayo Algeria walishindwa mabao 2-1 na Ujerumani katika muda wa ziada anasisitiza kuwa Saumu hakikuchangia kwao Kushindwa.Aidha M’Bolhi anasema kuwa wachezaji hao wamekwisha zoea kucheza hata wakiwa kwenye mfungo na hivyo haipaswi kutolewa kama sababu .Kabla ya mechi hiyo kulikuwa na ubishi baada ya kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic kukataa kuulizwa maswali kuhusiana na mfungo wa Ramadhan ambao ulikuwa umeanza jumamosi .Halilhodzic alikataa kufichua idadi ya wachezaji wake ambao wanafunga mfungo wa Ramadhan kabla ya mechi .Wakati uo huo kocha huyo alikataa kujibu swali ikiwa wachezaji wake watafunga Ramadhan au la wakati wakicheza.Kulingana na dini ya Kislamu ,Ramadhan ni nguzo muhimu ya dini na ifikapo wakati huo kila mtu mwenye umri wa baleghe hujinyima chakula kuanzia alfajiri hadi magharibi .Hiyo inaamisha kuwa wachezaji wa Algeria hawakuwa wamekula chochote hadi baada ya kipindi cha pili cha mechi hiyo ndipo waliporuhusiwa  kunywa na  kula .Ujerumani ilifuzu kwa robo fainali ya kombe la dunia ambapo watakutana na Ufaransa ijumaa ijayo.

Said PiePie,Nairobi.

KOCHA WA NIGERIA AFUNGANYA VIRAGO



Aliyekua kocha wa Nigeria almaarufu Super Eagles  Stephen Keshi 
      Stephen Keshi  Kocha wa Nigeria amejiuzulu baada ya timu ya Super Eagles kuondolewa kutoka kwenye kipute cha kombe la dunia walipozabwa 2-0 na Ufaransa .Keshi mwenye umri wa miaka 52 alichukua wadhfa huo mwaka wa 2011 na akaiongoza timu hiyo na kutwaa ubingwa wa afrika mwaka uliopita .Wakati uo huo nahodha wa timu hiyo Joseph Yobo aliyejifunga bao la pili la Ufaransa naye pia ametangaza kustaafu .Keshi chini ya uongozi wake Super Eagles imefuzu kwa mara ya kwanza katika mkondo wa pili wa kombe la dunia tangu mwaka wa 1998 licha ya kukumbwa na migomo ya wachezaji wake wakidai malimbikizi ya marupurupu.kocha waliojiuzulu kufuatia matokeo duni katika kombe la dunia kutimia makocha 6.Hadi sasa kocha wengine waliojiuzilu ni pamoja na Luis Suarez, wa Honduras, Carlos Queiroz wa Iran's ,Alberto Zaccheroni wa Japan , Cesare Prandelli wa italia na Sabri Lamouchi wa Ivory Coast.Hapo awali Keshi, aliwahi kuhudumu kama kocha wa Mali na Togo.

Said PiePie,Nairobi.