![]() |
Sam Nyamweya Mwenyekiti wa FKF |
Mwenyekiti
wa shirikisho la kandanda nchini Sam Nyamweya anamtaka Gavana wa Machakos Alfred Mutua aombe msamaha
kwa matamshi aliyoyatoa kuwa timu ya taifa ya
Harambee Stars hutumia magari aina ya Matatu kwa usafiri wake hii ni kulingana
na ripoti iliyochapishwa kwa mtandao wa shirikisho la FKF.Wakati uo huo Nyamweya alipinga
madai hayo akisema kuwa Harambee Stars hutumia usafiri waa ndege.Huku hayo yakijiri Stars wanapania
kumenyana na timu ya taifa ya Lesotho katika mchuano wa kufuzu katika mechi za
AFCON 2015 Julai 19 Maseru Lesotho huku mchuano wa nyumbani ukiratibiwa kucharazwa Agosti 3 mjini Nakuru.
Said PiePie,Nairobi
No comments:
Post a Comment