Stephen Keshi Kocha wa Nigeria amejiuzulu baada ya timu ya
Super Eagles kuondolewa kutoka kwenye kipute cha kombe la dunia walipozabwa 2-0
na Ufaransa .Keshi mwenye umri wa miaka 52
alichukua wadhfa huo mwaka wa 2011 na akaiongoza timu hiyo na kutwaa ubingwa wa
afrika mwaka uliopita .Wakati uo huo nahodha wa timu hiyo
Joseph Yobo aliyejifunga bao la pili la Ufaransa naye pia ametangaza kustaafu .Keshi chini ya uongozi wake Super
Eagles imefuzu kwa mara ya kwanza katika mkondo wa pili wa kombe la dunia tangu
mwaka wa 1998 licha ya kukumbwa na migomo ya wachezaji wake wakidai malimbikizi
ya marupurupu.kocha waliojiuzulu kufuatia matokeo duni katika kombe la dunia kutimia
makocha 6.Hadi sasa kocha wengine waliojiuzilu ni pamoja
na Luis Suarez, wa Honduras, Carlos Queiroz wa Iran's ,Alberto Zaccheroni wa
Japan , Cesare Prandelli wa italia na Sabri Lamouchi wa Ivory Coast.Hapo awali Keshi,
aliwahi kuhudumu kama kocha wa Mali na Togo.
Said PiePie,Nairobi.
No comments:
Post a Comment