Friday, 4 July 2014

BRAZIL KUMENYANA NA COLOMBIA



Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil alamaarufu Samba Boys
   B
razil na Colombia zitamenyana kwenye mchezo wa robo fainali ya  Kombe la Dunia hii leo mchuano huo utakaragaziwa  Uwanjani Castelao mjini Fortaleza.Mara ya mwisho Colombia kuilaza  Brazil ilikuwa mwaka 1991. Lakini, kipute hicho cha robo fainali ya Kombe la Dunia kinaikuta Colombia ikiwa kwenye ubora mkubwa na kuundwa na nyota makini akiwemo Rodriguez, Juan Cuadrado na Jackson Martinez na kuwafanya Brazil kuwa kwenye presha kubwa sana.Cuadrado, ndiye mchezaji aliyepiga pasi nyingi zilizozaa mabao kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia, akiwa amechangia mabao manne kwa kikosi cha Colombia.Kwenye hatua ya 16 bora, Brazil ilipata shida dhidi ya Chile na kufanikiwa kuwatupa nje kwa mikwaju ya penalti 3-2, wakati Colombia iliichapa Uruguay kiulaini mabao 2-0, shukrani kwa mabao hatari ya Rodriguez na kazi nzuri ya staa wa taifa hilo, Cuadrado.Utamu wa mchezo huo utazikutanisha timu mbili zinazobebwa na mastaa vijana, Neymar kwa upande wa Brazil na Rodriguez kwa Colombia. Kwenye fainali hizo, Neymar ametikisa nyavu mara mbili, moja pungufu ya mpinzani wake wa leo, James Rodriguez. 


Radamel Falcao Strika wa Colombia
Robo fainali hiyo itatanguliwa na ile kati ya Ufaransa na Ujerumani itakayopigwa kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro. Mechi hiyo ya Ufaransa na Ujerumani ni ya kihistoria.
Timu hizo mbili ziliwahi kumenyana kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 1982, ambapo Wajerumani walishinda kwa mikwaju ya penalti. Ufaransa itaingia kwenye mchezo huo ikitaka kulipa kisasi, lakini jambo hilo litafanywa na wachezaji 21 kati ya 23 kwenye kikosi hicho cha Les Bleus ambao walikuwa hawajazaliwa wakati timu yao ikifungwa kwa penalti na Ujerumani katika fainali hizo.Kiungo Blaise Matuidi atabeba majukumu ya Ufaransa kwenye sehemu ya kiungo sambamba na Paul Pogba na Yohan Cabaye, ambao watakuwa kwenye vita ya nguvu dhidi ya Toni Kroos, ambaye amefunika kwa kupiga pasi katika fainali hizo za Brazil.Aidha mechi nyingine za hatua ya robo fainali zitaendelea kesho,ambapo Argentina itakajimwaya uwanjani  na Ubelgiji na Uholanzi itakapokwaruzana na Costa Rica.


Said PiePie,Nairobi


No comments:

Post a Comment