Thursday, 26 June 2014

FIFA YAMPIGA MARUFUKU BECKNERBAUER



 
Aliyekua Kocha wa Ujerumani Franz Beckenbauer

           Franz Beckenbauer amepigwa marufuku ya siku 90 kujihusisha na soka kwa kushindwa kutoa ushikiano wake kwa kamati ya uchunguzi ya FIFA.
Aidha FIFA imedokeza kuwa Beckenbauer alikua katika  kamati kuu ya Shirikisho la Kimataifa la soka (FIFA) ambalo mwaka 2010 li iliwapatia Qatar kuandaa michuano ya michuano  ya Kombe la Dunia kwa mwaka 2022,aliombwa mara kadhaa kutoa maelezo yake kuhusu uamuzi huo tata.Marufuku hiyo imewekwa kufuatia ombi la mwanasheria wa Marekani Michael Garcia mkuu wa jopo la uchunguzi wa kamati ya maadili ya FIFA ambaye anaongoza uchunguzi kuhusu uamuzi huo wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022.
         Jumatano Garcia aliuambia mkutano mkuu wa FIFA wa kila mwaka mjini Sau Paulo Brazil kwamba yeye na kamati yake tayari walikuwa na sehemu kubwa ya mamilioni ya nyaraka ambazo zimetajwa na gazeti la Sunday Times la Uingereza katika repoti ya karibuni inayodai kutolewa kwa rushwa katika harakati za kufanikisha Qatar ipate nafasi ya kuandaa michuano hiyo ya soka Kombe la Dunia.
Gazeti la Sunday Times limesema baadhi ya mamilioni ya nyaraka imeziona kuwa zinahusiana na malipo yaliyotolewa na mjumbe wa zamani wa kamati kuu ya FIFA Bin Hammam kwa maafisa ikiwa kama sehemu ya kampeni ya kuungwa mkono kwa harakati za Qatar kuandaa michuano hiyo ya Kombe la Dunia.
Kesi hiyo hivi sasa iko kwenye taratibu rasmi za uchunguzi chini ya mjumbe wa jopo hilo Vanessa Allard akiwa kama mkuu wa uchunguzi.Repoti rasmi ya uchunguzi huo inatarajiwa kutolewa hapo mwezi wa Julai.

Said PiePie,Nairobi.

No comments:

Post a Comment