Tuesday, 17 June 2014

MAREKANI YAIZIMA GHANA




       John Brooks liliwapa Marekani ushindi uliotokana na kibarua kigumu wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Ghana katika uwanja wa Estadio das Nunas mjini Natal
Clint Dempsey alifunga goli la kasi sana na ambalo ni la tano katika historia ya Kombe la Dunia, na kuwaweka kifua mbele vijana wa kocha Jurgen Klinsmann baada ya sekunde 29.
Andre Ayew aliwapa pointi 1 Ghana almaarufu Black Stars  alipofunga bao safi baada ya kuandaliwa pasi  kisigino na Asamoah Gyan, wakati kukiwa kumesalia dakika 8 katika kipindi cha kwanza
Uzembe wa Ghana ulimpa fursa beki wa Marekani Brooks kufunga kichwa safi kutokana na mkwaju wa kona zikiwa zimesalia dakika 5 mpira kumalizika. Hilo lilikuwa goli lake la kwanza la kimataifa, na likampa ushindi Jurgen Klinsmann ambaye ameadhimisha mchuano wa 50 akiwa na timu ya taifa ya Marekani.

        
Shabiki wa Ghana na mbwembwe zake
Black Stars walitawala mchezo kwa muda mrefu lakini mwishoni walijuta kwa kushindwa kuzitumia fursa zao  kufunga mabao.Marekani sasa itacheza mchuano ujao dhidi ya Ureno, ambao walizabwa magoli 4-0 na Ujerumani, wakiwa na matumaini kuwa wanaweza kufuzu katika 16 za mwisho.
Kocha Klinsmann amesema “kuna mambo ambayo tunaweza kuimarisha lakini leo tumepata points tatu tulizozihitaji sana”. Aliongeza kuwa “Ghana ni timu nzuri na wanajua namna ya kuumiliki mchezo. Hilo lilitarajiwa”.
Kocha wa Ghana Kwesi Appiah alikanusha madai kuwa mchezo wa vijana wake ulitokana na mgomo baridi wa wachezaji lakini akakiri kuwa Black Stars bado wasubiri malipo yao kamili ya marupurupu.
Ghana walifika katika robo fainali ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka wa 2010, sasa wanakabiliwa na mlima mkubwa wa kuukwea ili kujiondoa katika kundi hilo ambalo lina Ujerumani, Ureno.
Marekani imelipiza kisasi cha kushindwa katika michuano miwili ya kombe la dunia na Ghana .

Said Piepie,Nairobi.

No comments:

Post a Comment