Wednesday, 25 June 2014

SUAREZ AMNG'ATA GIORGIO


 
Luiz Suarez aendeleza ukandamizaji
                   Strika wa  Uruguay Luis Suarez anakabiliwa na marufuku  itakayomlazimu kukosa mechi nyengine za michuano ya kombe la dunia iwapo atapatikana na hatia ya kumng'ata mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini katika mechi ya hapo jana.

Shirikisho la soka duniani FIFA limeanzisha uchunguzi wa kumuadhibu mcheza huyo kufuatia ushindi wa moja kwa bila dhidi ya Italy.
Chiellini amedai kwamba Suarez alimng'ata bega lake licha ya Suarez kudai kuwa ni mchazaji huyo aliyemchezea vibaya.

Giorgio Chiellini aonyesha jeraha baada ya kung'atwa na Suarez
  

Suarez mwenye umri wa miaka 27 huenda akapigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi 24 ama miaka miwili.
Refa aliyesimamia mechi hiyo kutoka Mexico Marco Rodriguez hakuchukua hatua yoyote kufuatia kisa hicho,lakini FIFA bado inaweza kumuadhibu Suarez.
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Liverpool Jan Molby anatarajia kwamba Suarez atapigwa marufuku kwa mechi zote za kombe hilo zilizosalia.



Said PiePie,Nairobi.

LAMOUCHI AGURA IVORY COAST



Aliyekua kocha wa Ivory Coast Sabri Lamouchi


        Kocha wa Ivory Coast Sabri Lamouchi amejiuzulu baada ya timu yake kuzabwa 2-1 na Ugiriki hapo jana katika mechi ya kuisismua
Lamouchi aliliambia jarida la AFP katika mahojiano jana baada ya mechi hiyo kumalizika aidha raia huyo wa Ufaranza mwenye umri wa mika 42 amesema kuwa kandarasi yake ilimalizika jana.
Hata hivyo amedokeza kuwa kushindwa kwake kulichangiwa na mchezo duni ambao wachezaji wake walionyeshwa baada ya kupoteza fursa tumbi nzima waliopata.Lamouchi ilianza kuwaongoza Ivory Coast mnamo Mei 2012.

Said PiePie,Nairobi.




MECHI ZA KPL ZAHAIRISHWA


                             

        Mechi saba za ligi ya primia humu nchini  zilizokuwa zimeratibiwa kusakatwa wikendi hii zihairishwa.Kulingana na afisa mkuu ya Ligi ya primia nchini Jack Oguda amesema kuwa hali hii imechangiwa na kusafiri kwa kikosi cha Harambee Stars  kuelekea Brazil
Aidha Oguda ameongeza kuwa michuano ya ligi ya primia itarejelewa kuanzia Jumamosi tarehe 5 Julai na Jumapili 6 mwezi ujao.


Said PiePie,Nairobi.

Tuesday, 24 June 2014

SOFAPAKA YAPATA MLINDALANGO MPYA




 Mutuyimana mlindalango wa Kiyovu Sports

   Timu ya Sofapaka almaarufu Babatoto ba Mungu imekubali kumsajili mlinda lango  kutoka timu ya taifa ya Rwanda anayetokea klabu ya Kiyovu sports
Kulingana na mwenyeketi wa Sofapaka Elly Kalekwa kupitia mtandao amesema majadiliano rasmi yanaendelea na hivi karibuni mlinda lango huyo atajiunga nao.Kuwasili kwa  Mutuyimana katika klabu ya sofapaka kutasaidia pakubwa  kwani kipa wao Duncan Ochieng’ kwa sasa bado anauguza jeraha.

Said PiePie,Nairobi

Monday, 23 June 2014

ORIGI ANG'ARA BRAZIL




Origi anayesakatia kabumbu taifa la Ubelgiji na Lille ya Ufaransa.
          Divock Origi amemshukuru babake mzazi kwa kuhudhuria mechi ya hapo jana dhidi ya Urusi, jambo ambalo amesema lilichangia pakubwa ushidi  wao wa jana,huku Ubelgiji ikijiaandika nafasi katika 16 bora katika michuano ya kombe la dunia inayo endelea kule Brazil.Kwa sasa Ubelgiji inaangoza kundi la HA na alama 6.
Hapo awali Origi ilichezea timu za  U15, U16, U17 na U19 zote za  Ubelgiji  huku akifunga bao lake la kwanza kwa ka timu ya U19 katika mechi za UEFA 2013
Ubelgiji walizaba Urusi 1-0.


Said PiePie, Nairobi.